23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wanaohujumu miradi waonywa

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Huduma za Meli, Profesa Zacharia Mganilwa amewataka wananchi kuacha kudokoa, kuchomoa na kuiba vifaa kwenye miradi inayotekekezwa nchini badala yake wafanye kazi kwa uaminifu na kujituma kwa bidii ili waweze wanajipatia kipato kwenye familia zao.

Prof. Mganinilwa amesema hayo Mei 26, 2021 wakati wa hafla ya kusaini mkataba na Kampuni ya Korea kusini Total Marine Innovation (KTMI) kwa ajili ya ukarabati wa meli ya Mt. Sangara na kiusema kuwa ukarabati wake unatyarajiwa kukamilika kabla ya miezi 12 ili wananchi waendelee kunufaika na miradi hiyo.

Amesema ni vema wananchi ambao watapata fursa kwenye mradi huo kujishughulisha kwa bidii na uaminifu ili kuboresha maisha yao kwani zaidi ya watanzani 200 wananufaika  na mradi huo kwa kupata ajira za kudumu na za muda mfupi.

Amefafanua kuwa mradi huo wa ukarabati wa meli utaghalimu dola za kimarekani milioni 3.6 sawa na Sh bilioni 10 kwani bajeti ya mwaka wa fedha ni Sh bilioni 134 ambayo imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya nne na ukarabati wa meli tatu kwani Mt. Sangara iliyohalibika Oktoba mwaka jana ilikuwa ikisafiri kutoka Kigoma kwenda nchi za Burundi hadi Kongo DRC.

“Kampuni hii ina jumla ya melimi 14 ambazo zote zitakarabatiwa na kutakuwa na ujenzi wa meli mpya ambapo katika ziwa Viktoria tutajenga mbili, ziwa Tanganyika tutajenga meli ya abilia naye mizigo na bahari tutajenga itakayobeba mizigo tani 3,500 kwani hizi ni juhudi zinazotokana na serika ya awamu ya tano na sita,”amesema Mganilwa.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya huduma za meli, Philemon Bagambilana amesema meli hiyo ya Mt. Sangara yenye uwezo wa kubeba mafuta lita 410,000 kwa wakati mmoja kwani aliyeshinda zabuni ya ukarabani  ni mzoefu kwani alijenga meli ya Mv Butiama na Mv Viktoria kuongeza utendaji kazi wao na kutumia miezi michache katika ukarabati huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles