31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAMTAKA ZAMBI KUINGILIA MGOGORO SHAMBA LA DEWA

Hadija Omary, Lindi

Wananchi wa Kata ya Kiwalala, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi mkoani hapa, wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuingilia kati mgogoro wa shamba lijulikanalo kama Shamba la Dewa kwa madai ya uwepo wa wananchi wachache kunufaika nalo isivyo halali.

Kwa mujibu wa Diwani wa kata hiyo, Mohamed Chakale amesema kuwa shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 1,500 kwa sasa ni mali halali ya mwekezaji ajulikanae kwa jina la Dewa.

Amesema shamba hilo alilitelekeza miaka ya 20 iliyopita ambapo serikali iliamua kuligawa kwa wananchi kwa masharti ya kutopanda mazao ya kudumu.

“Baada ya Halmashauri ya Kijiji kupitia vikao vya maendeleo ya kata kuamua kuligawa shamba hilo kwa wananchi wengine kwa kuchangia Sh 50,000 ili kujiongezea kipato katika serikali yao ya kijiji.

“Shamba hili liliachwa na mwekezaji miaka ya 1998 likiwa limepandwa mikorosho Mkuu wa Mkoa wa wakati ule akaamrisha kupitia vikundi wananchi walihudumie shamba hilo mpaka mmiliki atakaporejea na atatakiwa kuwalipa fidia wananchi watakaolihudumia shamba hilo kwa kipindi chote ili lisiendelee kuwa pori,” amesema Chikale.

Akizungumzia mgogoro huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amepiga marufuku kwa wananchi kufanya shughuli za kilimo na matumizi mengine katika shamba hilo.

“Namuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, kumchukulia hatua za kisheria yeyote atakayekaidi agizo hili,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles