26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, January 27, 2022

WANANCHI WAMLILIA JPM WASIHAMISHWE

Na LILIAN JUSTICE, MVOMERO


WANANCHI wa vijiji vya Kunke na Mlumbilo wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, wamemuomba Rais Dk. John Magufuli kuwasaidia ili wabakie  kwenye maeneo yao.

Hatua hiyo imetokana na agizo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kutoa tamko la kuwataka kuhama ifikapo Agosti 30, mwaka huu, kwa kile kinachodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi.

 

Wananchi hao walitoa ombi hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika vijiji hivyo na kutoa kilio chao mbele ya Diwani wa Kata ya Mtibwa, Lucas Mwakambaya.

Baadhi ya wananchi hao, Hassan Suleman, mkazi wa Kitongoji cha Mafleta B –Pagale alisema kuna waraka umesambazwa kuwataka wajiandae kuhama kwa madai wamevamia msitu wa hifadhi wa Pagale.

 “Tumekaa hapa muda mrefu kabla ya msitu wa hifadhi kuwekewa mipaka mwaka 1952 na wakoloni, tunashangaa kuambiwa tuhame bila ya kuitishwa mkutano kuelezwa rasmi,” alisema Suleman.

Naye Enedius Mpesa,  mkazi wa Kitongoji cha Masangarawe, Kijiji cha Mlumbilo, alisema wanatekeleza agizo la Rais Dk. Magufuli la kutoitegemea Serikali kuwapa msaada.

Naye Diwani Mwakambaya aliwaomba wawe watulivu kwa sababu Serikali ni sikivu na jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake, Meneja Hifadhi ya Misitu Wilaya ya Mvomero (TFS),  Husna Msagati, alipoulizwa kuhusu sakata hilo aliwaondoa hofu wananchi hao kuwa wao hawana lengo la kumfukuza mwananchi, bali wanatekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, la kuhakikisha maeneo ya hifadhi za misitu yanapimwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,803FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles