25.1 C
Dar es Salaam
Monday, October 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wamiminika banda banda la JKCI, wanywa bia waonywa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imesema hadi kufikia Julai 8, mwaka huu jumla ya Watanzania 525 wamejitokeza kupima afya kwenye banda lililopo kwenye maonyesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa sabasaba.

Akizumgumza leo Julai 9 na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge amesema kuna madaktari bingwa wa moyo na wauguzi wazoefu wapo kwenye maonyesho hayo wananchi wakipime afya zao.

Amesema Tiba Utalii imesababisha kupokea wagonjwa wengi kutoka nchi 20 zinategemea kupata huduma katika taasisi hiyo.

“Kuwepo kwenye maonyesho haya moja ni kufanya vipimo kwa wagonjwa na kuonyesha huduma mbalimbali tunazofanya hadi kufikia Julai 8, wananchi waliojitokeza ni 525 vipomo vya ECO 95, umeme wa moyo 83, rufaa 37 na vipimo vya maabala 58,” amesema Dk. Kisenge.

Amesema wamekuwa na uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba vya hali juu ili kuwezesha kutoa huduma kwa wakati.

Amesema katika asilimia 25 yote ya magonjwa ya moyo yanaongezeka kutokana na watu kutokufanya mazoezi pamoja na vyakula.

Katika hilo Dk. Kisenge amewashauri Watanzania kwa wale ambao ni wanyaji wa pombe kunywa bia tatu angalau kwa sikuna wapunguze kula vyakula vya wanga, kutumia sukari nyingi ili kupunguza magonjwa ya moyo huku akiwashauri kula matunda kwa sana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles