26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wala fisi kupoza machungu

Na Allan Vicent, Kaliua

Wananchi wenye hasira wamemgeuza kitoweo fisi aliyeingia ndani ya nyumba na kunyakua mtoto anayeitwa Mazoya Nghanya (1) na kukimbia naye porini na kusababishia kifo chake, huku akijeruhi watu  watatu walikwenda kumwokoa.

Wakizungumzia tukio hilo lililotokea Julai 25,2021, saa 9 usiku katika kijiji cha Kangeme kata ya Zungimlole Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora baadhi ya wakazi wa kata hiyo wameeleza kuwa baada ya fisi huyo kuuawa na askari wa Maliasili kwa kushirikiana na Polisi kwa hasira wameamua kula nyama yake ili kupoza machungu.

Mkazi wa kata hiyo Joshua Msandeke (45), amesema ni kweli fisi huyo mla watu na yeye ameliwa na wananchi wenye hasira ili kupoza machungu ya kupoteza mtoto wao na kujeruhiwa ndugu zao.  

Amebainisha kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya kukasirishwa na kitendo cha mnyama huyo kuua mtoto wao, kuwasumbua na kujeruhi wenzao watatu waliokuwa wakiokoa maisha ya mtoto.

Hamisi Kenyela mkazi wa Kangeme ameeleza kuwa wanakijiji wana uchungu  ndio sababu wameamua kugawana nyama yake na kuila,  wakiongeza kuwa fisi wamekuwa wakisumbua wakazi wa kijiji hicho kilicho karibu na hifadhi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Kamishna Msaidizi Safia Jongo, amesema kuwa tukio hilo lilitokea katika hifadhi ya Luganzo -Tongwe Kijiji cha Kangeme kata ya Zugimlole.

Amesema  licha ya askari kupambana na kufanikiwa kumuua lakini walipoteza risasi zipatazo 49 kwa kumpiga hadi walipofanikiwa kumuua.

Amewataja waliojeruhiwa na mnyama huyo kuwa ni baba wa mtoto aliyeuawa, Nganya Mayala (45) ambaye aling’atwa kwenye kiganja cha mkono wa kulia, Ngezi Lega (25) aliyeng’atwa mkono wa kushoto na paja na Tule Malongo (45) aliyevunjwa taya na kung’atwa mkono wa kushoto hadi sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles