27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAJENGA SHULE LINDI

Hadija Omary, Lindi

Changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wanaoishi katika Mtaa wa Mitwero, Kata ya Rasibura Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imepata mwarobaini baada ya wananchi wa kata hiyo kuamua kujenga shule ya sekondari katika mtaa huo.

Awali, wanafunzi hao walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 10 kwenda shule kutoka Mitwero kwenda Shule ya Sekondari Lindi na Mkonge.

Ujenzi huo wa shule, umetokana na nguvu za wananchi baada ya kata hiyo kukosa shule ya sekondari katika mtaa huo ambao uko nje ya Mji huo Lindi na kuwalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Jomari Satura amesema shule hiyo kwa sasa ina wanafunzi 159 ambao wana mikondo mitau, vyumba vya madarasa sita na matundu ya vyoo 13.

“Ujenzi huu wa shule pamoja na vifaa vya kujifundishia, vitabu na vifaa vingine umeghalimu kiasi cha fedha tasilimu cha Sh milioni 150 huku nguvu za wananchi pekee zikiwa Sh milioni 194,” amesema.

Akizindua shule hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kupata mafanikio huku akisisitiza ushirikiano baina ya walimu, wanafunzi na wazazi katika kuinua kiwango cha elimu mkoani hapo

Aidha zambi amewataka wanafunzi na walimu kuyatunza majengo na vifaa vya shuleni hapo ili vidumu na kutumika kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles