23.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wahimizwa kuwekeza Faida Fund

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Watumishi Housing Investment imejivunia kukua kwa mfuko wa uwekezaji wa Faida Fund na kuendelea kuwavutia wawekezaji wengi kutokana na mfumo wanaotumia ikiwamo kiwango cha fedha cha uwekezaji walichoweka.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Investment, Dk. Fred Msemwa, leo Agosti 6, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari,jijini Dar es Salaam kuhusu mkutano mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Agosti 10, 2024 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere (JNICC)..

Amesema tangu kuanzishwa kwa mfuko wa Faida Fund mtaji wake umekuwa tofauti na walipoanza kipande kilikuwa kina thamani ya sh. 100 lakini sasa ni sh. 117.

“Kiwango chetu kuanzia kuwekeza kimechochea uwekezaji katika soko la fedha, tuna wawekezajj wadogo ambao wanaweza kuwekeza kuanzia Sh.10,000 na wakaendelea kuwekeza wakiwa na 5000.

“Kushusha kwa kiwango cha uwekezaji umeweza kuanzishwa kwa mifuko mingine ya uwekezaji katika soko la fedha. Pia Tumebuni mfumo ambao unawezesha wawekezaji kuwekeza na kupata faida na kuuza vipande vyake bila kufika ofisini kujaza fomu.

Ameeleza kuwa wakati wakitimiza mwaka mmoja mfumo huo umeweza kufikia hata watu waliopo kijijini, wanaonufaika na huduma hiyo.

Kwa upande wake Marry Mponda kutoka CRDB ambaye ni mwangalizi wa mfuko huo amewatoa hofu wawekezaji na kusema fedha zao ziko sehemu salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles