27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Tarime wapeleka kilio cha fidia kwa Rais Magufuli

Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Na JONAS MUSHI-DAR ES SALAAM

WANANCHI wa Kitongoji cha Nyamichere, Kijiji cha Nyakunguru wilayani Tarime mkoani Mara, wametoa kilio chao kwa Rais John Magufuli na kumwomba atekeleze ahadi yake ya kutatua mgogoro kati yao na mgodi wa North Mara/Accacia.

Wawakilishi wa wakazi hao ambao wapo zaidi ya 1,000, walifunga safari kutoka Mara hadi  Dar es Salaam na kuzungumza na waandishi wa habari jana kuhusu madhila wanayoyapata katika ulipwaji wa fidia.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Samwel Timas, alisema wameamua kufikisha kilio chao kwa Rais Magufuli baada ya kuwepo kwa njama za kupunguza kiasi cha fidia wanayotakiwa kulipa kwa kubadilisha tathmini waliyofanyiwa awali.

Alisema baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila malipo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliunda tume ambayo hatimaye iliona kuwa mgodi hauhitaji tena eneo hilo na kupendekeza wananchi wawe wamelipwa fidia ya mazao na ya usumbufu hadi ifikapo Septemba 30, mwaka huu.

“Pendekezo la Tume ya Profesa Muhongo ambalo lilisomwa kwa wananchi Julai 20 mwaka huu, mbele ya waziri lilieleza kuwa maeneo yaliyofyekwa mazao na baadaye ikabainaka kuwa mgodi hauhitaji maeneo hayo, wananchi wanapaswa walipwe fidia ya mazao na usumbufu,” alisema Timas.

“Mapendekezo haya yalikubaliwa na wananchi wote na likatolewa agizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga, asimamie utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kutoa nakala ya mapendekezo hayo kwa vijiji husika.

“Cha kushangaza siku mapendekezo hayo yalipogawiwa kwa kila kijiji, ilibainika kuwa kipengele kilichoelekeza tulipwe kadiri ya mazao yaliyofyekwa, kilibadilishwa na kusomeka kuwa ‘wananchi walipwe kulingana na upandaji bora wa mazao,” alisema Timas.

“Tunamwomba Rais Magufuli aingilie kati suala hili kwani aliahidi siku anapiga kampeni Septemba 11 mwaka jana, tulimsimamisha eneo la Nyamwaga na kumwonyesha mabango na akasema ametuelewa na akifika Ikulu atamaliza mgogoro huo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles