WATU zaidi ya 60,000 wamekimbia makazi yao Sudan Kusini tangu machafuko ya siasa yaanze tena wiki tatu zilizopita.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) iliyotelewa jana imesema.
Msemaji wa UNHCR, Melissa Fleming, alisema: “Wametuletea ripoti ya kusikitisha ya makundi ya waasi wanaojificha kwenye barabara inayokwenda Uganda ambao wanawazuia watu wanaokimbia.
“Waasi hayo wanavamia vijiji, wanaua raia na kuwalazimisha vijana wadogo kujiunga na kundi hilo”.
Taarifa za Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) zinasema waasi wengi wamekuwa wakienda kwenye mpaka wa Uganda katika siku 10 zilizopita na wengine wanakwenda Sudan na Kenya.