23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Nkasi waiomba Serikali nishati safi na salama ya kupikia

Na Mwanadishi Wetu, Mtanzania Digital

Wananchi mbalimbali katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wameiomba Serikali kuwapatia nishati safi na salama ya kupikia ili waweze kufanya shughuli za kuwaingizia kipato ikiwemo ukaangaji wa Samaki na Dagaa bila kuathiri afya zao kutokana na moshi.

Maombi hayo yametolewa kwa nyakati tofauti wakati Waziri wa Nishati, January Makamba alipofanya ziara katika Kijiji cha Kilando na Kisiwa cha Mandakelenge wilayani Nkasi ili kusikiliza kero za wananchi, kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kukagua usambazaji umeme katika Kisiwa cha Mandakelenge ambacho kinapata umeme baada ya Serikali kupitisha nyaya za umeme chini ya maji katika Ziwa Tanganyika .

Gerald Muta Kutoka Kisiwa cha Mandakelenge amesema pamoja  na kushukuru Serikali kuwapelekea umeme kwenye Kisiwa hicho, alimuomba Waziri wa Nishati kuwawezesha Kinamama Wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia ili wafanye kazi ya kukaanga samaki na dagaa kwa wingi kwani kisiwa hicho kwa sasa kina uhaba wa kuni na mkaa.

Mbele ya Waziri wa Nishati, Zurietha Msarange kutoka Kisiwa cha Mandakelenge amesema: “Tunakuomba Mhe Waziri utuwekee miundombinu ya kisasa ya kupikia ili tujiwezeshe kufanya biashara ya samaki na kuuza maeneo mengine hali itakayotuongezea kipato,” amesema Zurieth.

Waziri wa Nishati amesema kuwa upatikanaji wa kuni na mkaa ni changamoto kwenye Visiwa kwani unaweza kusababisha visiwa hivyo kuwa jangwa na kwamba maeneo kama hayo yanapaswa kuwa mfano wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

Katika kutekeleza ombi hilo la upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia, Waziri wa Nishati alitoa mitungi 50 kwa vikundi mbalimbali vya kina mama lishe  na kueleza kuwa huo ni mwanzo wa safari ya kufikia mahala ambapo kila nyumba nchini itatumia nishati safi ya kupikia isiyotoa moshi ambao una athari kwa afya.

Mkoa wa Rukwa una vijiji 339 na tayari vijiji 199 vimeshasambaziwa umeme na kuahidi kuwa vijiji vyote vilivyosalia vitasambaziwa umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles