26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wananchi Ngulugulu waomba Barabara wasafirishe Tangawizi

Na Denis Sinkonde, Songwe

WANANCHI wa kata ya Ngulugulu wilayani Ileje mkoani Songwe wameiomba Serikali kuwakarabatia barabara ya Vimetu kwenda Lema yenye urefu wa km 30 ili kuwaondolea adha ya muda mrefu ya kusafirisha zao la Tangawizi ambalo kwa mwaka sasa hawajavuna zao hilo.

Wananchi hao walitoa ombi hilo jana kwa Mbunge wa Jimbo la Ileje na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Geodfrey Kasekenya Msongwe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ngulugulu kata ya Ngulugulu wilayani hapa.

Wananchi wakifuatilia mkutano huo.

Edisoni Mlwafu Mkazi wa kijiji hicho alisema kutokana na barabara hiyo kuwa tegemezi kiuchumi katika kusafirisha zao la Tangawizi ni mwaka sasa hawajavuna zao hilo mashambani kutokana na magari ya wananuzi kutofika mashambani hali ambayo imesababisha kushusha bei ya zao hilo kwa wananchi wa kata hiyo hususan wananchi wa kijiji cha Kisyesye.

“Uchumi wetu si mzuri kwani sisi tunategemea zao la Tangawizi lakini toka mwaka 2021 hatujawi kuvuna, tatizo kubwa likiwa ni ukosefu wa barabara ambayo ingewarahisishia wanunuzi kuingia shambani kwa kutumia magari kununua zao hilo,” amesema Mlwafu.

Enita Kamwela amesema ili kuokoa uchumi wa wananchi hao ni muhimu serikali itenge bajeti ya kulima barabara hiyo itakayorahisisha kusafirisha zao hilo, sambamba na kuwasaidia kuwatafutia makampuni yatakayonunua zao hilo kwa bei nzuri ya kumnufaisha mkulima.

Kaimu Meneja wa TARURA wilayani hapa, Mhandisi Savali Ladson akizungumza katika mkutano huo kujibu kero hiyo ya wananchi, amesema tayari wamepokea fedha ya dharura  Sh milioni 100 kwa ajili ya kukarabati barabara hiyo ili kuondoa adha hiyo.

Mbunge wa Ileje Mhandisi Geodfrey Kasekenya amesema kutokana na changamoto ya wanachi kukosa soko la uhakika atashirikiana na idara ya kilimo kuwatafuta wadau watakaonunua zao la Tangawizi kwa lengo la kumnufaisha mkuluma kwani asilimia 90 ya wakazi wa Ileje hutegemea zao hilo.

“Serikali itahakisha inatatua changamoto ya soko la uhakika ili wananchi wanufaika sambamba na kulima barabara yenye urefu wa Km 30 ili wasafirishe zao hilo,” amesema Msongwe.

Mhandisi Msongwe amesema kutokana na changamoto hiyo atahakikisha wanashirikiana na wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA Ileje ili kuondoa changamoto zinazokwamisha uchumi kwa wananchi ikiwepo kuzifungua na kuweka lami nyepesi barabara ambazo ni muhimu huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles