28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wananchi Muleba waboreshewa miundombinu ya barabara

Renatha Kipaka, Muleba

Wananchi wa Kijiji Ccha Kimea na Kyamworwa kata Kasharunga Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamepata tumaini la kupunguza umbali wa kuzunguka kijiiji cha Runazi, Mushasha, hadi Nkomero kupata huduma za jamii baada ya wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kufungua Barabara ya Kyamworwa hadi Kimea.

Baadhi ya wananchi hao juzi wakiwamo, Jumaa Adinani, Jushua Tito, wamesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupunguza umbali wa kutembea zaidi ya Kilometa 20 kutoka kijiiji cha Kimea kwenda Kyamworwa ambapo kuna huduma mbalimbali za jamii.

Adinani ambae nimkazi wa kijiji cha kimea alisema tatizo kubwa lilikuwa pindi mama mjaziito anapofikia muda wa kujifungua katika kituo cha afya hulazimu kuzunguka vijiji vitatu.

Amesema kuwa mzunguko huo ilikuwa ni kulahisisha na kupata njia rahisi na yenye kufika eneo ambalo anatakiwa kwenda bila kujali garama za usafiri.

“Mtu anazunguka kutoka kimea Runazi, kasharunga, hadi kufikia Nkomero ndiyo apate huduma ya afya kwani sehemu nyinge ya Karibu kuna kinjia cha Enzi hakuna gari inayopita huko,” amesema Yahaya.

Naye Tito kutoka kijiji cha Kyamworwa amesema, nyakati za masika njia hiyo ilikuwa inajaa maji mifugo ikipitishwa kuna kuwa na hali ya kuteleza.

“Mfano ukitaka kutumia hiki kinjia cha shida shida utalipia Sh 2,000 kwa pikipiki, gari 1,000 lakini ukizunguka kwenye vijiji jirani hapa katikati utalipia Sh 3,000 hadi Sh 4,000,” amesema.

Mratibu wa Wakala wa Barabara mijini na Vijiji (TARURA) Mkoa wa Kagera, Avit Theodory amesema tayari Mkandarasi ameanza ujenzi wa barabara kuanzia Kimea hadi Kyamworwa.

Aidha, amesema Barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha changarama kwa gharama ya Sh milioni 474 kwa kufanya shughuli zote hadi kukamilisha na kusaidia kuondoa umbali km 21 walizokuwa wakitumia kutembea wananchi.

Amesema, baada ya kukamilika Mwananchi atatumia umbali wa km 9.8 pekee kutoka kata Kimea kwenda Kyamworwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles