26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WANANCHI MTWARA WAHIMIZWA KULIPA KODI YA ARDHI

Florence Sanawa, Mtwara

Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kusini, Gasper Luanda amewataka wananchi wanaomiliki ardhi mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kulipa kodi kabla ya Juni mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 17, amesema umiliki unaozungumziwa ni ule wa mwananchi kupewa nyaraka na serikali (hati au barua ya toleo) inayomthibisha kuwa yeye ndiye anayetambulika kumiliki kipande cha ardhi yaani kiwanja ama shamba.

“Wamiliki wote wa ardhi wamepewa masharti ya kutumia kiwanja ama shamba husika kwa kulipia kodi kila mwaka ambayo iko kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 na 33.

“Kodi hiyo hutakiwa kulipwa kwa hiari kuanzia Julai Mosi, hadi Desemba ya kila mwaka ambapo kuanzia Januari huanza kulipwa pamoja na faini ambayo ni asilimia moja kwa kila mwezi wa kodi husika,” amesema.

Hata hivyo, Luanda amesema mmiliki anayelimbikiza deni la kodi hii huchukuliwa hatua ikiwamo kufikishwa mahakamani Sheria ya Ardhi Sura ya 113.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles