29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Maswa wampongeza rais magufuli kwa ujenzi wa barabara

Samwel Mwanga – Maswa

Wananchi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa ziara yake mkoani humo mwaka jana ya kuwajengea barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 1.5.

Wakizungumza Mtanzania leo Mei 22 mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua barabara hizo wamesema wameridhishwa na kasi ya ujenzi ya barabara hizo zilizosimamiwa na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) ambazo zimewekewa taa ili zitumike pia nyakati za usiku.

‘’Tunamshukuru rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake alipokuwa wilayani Maswa na sisi kama wananchi tunamwahidi tutaitunza na kuifanyia usafi ili idumu kwa muda mrefu na wananchi waone manufaa ya barabara hizi za  mitaa,’’ amesema Mercy Emmanuel.

Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mkogea Ally amewashukuru viongozi wa serikali katika wilaya hiyo kwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hiyo uliozingatia viwango vya kiuhandisi na kufikia asilimia 98 ya ujenzi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles