30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

WANANCHI KUUNGANISHWA MTANDAO WA MAWASILIANO

Na ESTHER LEMA (OUT)-DAR ES SALAAM


WANANCHI wenye uwezo na wasiokuwa nao, wataunganishwa na mtandao wa mawasiliano kwa gharama nafuu zaidi na mtandao unaoongoza nchini wa Vodacom Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa kampuni hiyo Kanda ya Kaskazini, Henry Tzamburakis, wakati wa promosheni ya simu za kisasa za Smart Bomba zenye laini mbili ambazo zilizinduliwa na kampuni hiyo hivi karibuni.

Alisema tangu walipozindua promosheni hiyo kumekuwepo na mwitikio mzuri wa wananchi ambao wamekuwa wakizinunua simu hizi ili kuingia katika ulimwengu wa kidijitali.

 “Smart Phone mbali na kuwa na unafuu wa bei pia inaambatana na ofa ya mteja anayenunua simu kuunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za bure kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi mitatu  mfululizo kumwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote.

“Wakati ni huu kwa wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na maeneo ya jirani pamoja na mikoa mingine ya kanda hii kuchangamkia fursa hii ya kipekee kwa kununua simu ya Smart bomba kwa gharama nafuu na  kufurahia mawasiliano ya kisasa,” alisema Tzamburakis.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa promosheni ya mauzo ya simu hizo inayoendelea nchi nzima, baadhi ya wananchi wamesema hatua ya kampuni hiyo kuingiza sokoni simu za kisasa za Smart bomba zinazopatikana kwa gharama nafuu, imedhihirisha dhamira ya kweli ya kampuni hiyo ya kuwapeleka Watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles