29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI KUNDUCHI HATARINI KULIWA NA MAMBA

Na CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM


WAKAZI wa Kata ya Kunduchi maeneo ya Ununio, Dar es Salaam, wapo hatarini kuliwa na mamba aliyekuja na mvua za mafuriko na kuweka makazi katika madimbwi ya maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu.

Akizungumza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo, Diwani wa kata hiyo, Michael Urio (CCM), alisema eneo hilo ni hatarishi kwa watu kwani hadi sasa haijajulikana mamba hao wapo wangapi.

Alisema inawezekana mafuriko hayo yatakuwa yalileta yai la mamba mmoja au wawili na kuja kuzaliwa katika dimbwi hilo.

Diwani Urio, aliiomba Serikali kupitia wizara yenye dhamana kuchukua hatua kulipatia ufumbuzi suala hilo na kulifanya kama mradi wa dharura kuyaondoa maji hayo na kutengeneza mtaro huo ili wananchi wasidhurike.

“Maji haya yaliyotuama hapa yanatoka katika mfereji alimaarufu kwa jina la JK ambayo maji yanatoka katika sehemu mbalimbali, ikiwemo Boko Basihaya, Wazo hadi Ununio, ambayo yanapita katika mkondo wa maji na kutua katika viwanja vya watu,” alisema Urio.

Aliiomba Serikali kuu isaidie suala hilo ikiwamo kufuta baadhi ya viwanja ili mtaro uweze kutengenezwa katika viwango vinavyostahili.

Urio alisema hadi sasa mamba huyo hajaleta madhara yoyote licha ya watoto kucheza katika maji hayo.

Wakati huo huo, Urio alitembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa barabara kutoka Tegeta Stendi hadi Mtaa wa Kondo Bahari Beach.

“Mkandarasi wa barabara tunaomba aharakishe matengenezo hasa katika kipande hiki cha Stendi ya Tegeta ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara zao,” alisema Urio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles