23.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 25, 2021

Wananchi Kilema wakabiliwa na ubovu wa miundombinu

Na Upendo Mosha,Moshi

Wananchi wa Kijiji cha Marawe kyura, kata ya Kilema Kusini, wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ubovu wa miundombinu ya barabara hali ambayo imesababisha wanawake wajawazito kujitufungulia njiani na wanafunzi kushindwa kwenda shule kwa wakati.

Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa jimbo la vunjo (CCM), Dk.Charles Kimei, wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, katika kata hiyo, ambapo alisema,barabara ya Kilema Pofu imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi.

Alisema barabara hiyo yenye urefu wa zaidi ya kilometa nane imekuwa ni kero kubwa kutokana na kushindwa kupitika katika kipindi cha msimu wa mwaka mzima ambapo zaidi ya shilingi bilion nane zinahitajika kuijenga kwa kiwango cha lami.

“Barabara hii ya Kilema pofo imekuwa ni mbovu na inaleta shida kubwa kwa wananchi haswa wanawake wajawazito na wanafunzi…bahati mbaya wanajua Kilimanjaro tupo vizuri kwenye miundombinu Ila sio kweli, barabara hii ni mbovu na zinazohitajika ni bilion nane ili ijengwe kwa kiwango cha lami,”alisema Dk.Kimei

“Hii barabara ya kilema Pofo kwenda Mandaka ni barabara ambayo nimekuwa nikiizungumzia sana ila kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 fedha iliyotengwa ni milioni 254 fedhla ambayo haifiki popote kwenye ujenzi,maendeleo ya Kilimanjaro yataletwa na wananchi wenyewe Ila lile linalopaswa kufanywa na serikali lifanywe na serikali”alisema

Akizungumzia miradi mwingine ikiwemo ya afya, elimu na maji bado anaendelea kufanya jitihada za kuifuatilia na kupatikana kwa fedha zitakazo kamilisha miradi hiyo ambapo aliwataka wananchi kuendelea kushiriki katika u hangiaji wa miradi hiyo.

“Nimetembelea miradi mingi leo ikiwemo ya elimu,afya na ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Marawe lakini rai yangu naomba wananchi kushirikiana na mimi Mbunge wao washiriki kuchangia kwa nguvu na mali miradi hii kwa manufaa na maendeleo ya jimbo letu wote”alisema Dk.Kimei

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mrereni, Isere Thomas, alisema changamoto ya ubovu wa barabara hiyo imekuwa ni kero kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu jambo ambalo limechangia baadhi yao kukatisha masomo baada ya kupata vishawishi na kupata ujauzito.

Nao baadhi ya wananchi waliiomba serikali kuharakisha mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kutenga fedha zinazohitaji ili kuokoa maisha ya wanawake wajawazito na wanafunzi wakike wanaopata ujauzito kutokana na vishawishi baada ya kukaa muda mrefu barabarani.

“Barabara hii imekuwa kero idadi ni kubwa wanawake wanaojifungulia njiani kutokana na ubovu wa barabara na jambo baya zaidi imeathiri hadi watoto wetu wakike kukatisha masomo baada ya kupata ujauzito maana wanapata vishawishi”alisema Janeth Mwariko, Mkazi wa Kijiji cha Marawe

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,038FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles