22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Wananchi Kata ya Ijumbi Muleba kupata Mahakama

Na Kulwa Mzee, Muleba

Wananchi Kata ya Ijumbi, wilayani Muleba wanatarajia kupata Mahakama baada ya jengo lililopo kuwekwa kwenye mpango wa kukarabati mara Bunge la Bajeti ya mwaka 2021/2122 litakapomalizika.

Akizungumzia jengo hilo muda huu Afisa Mtendaji Kata, Salehe Mruma amesema viongozi wa Mahakama walitembelea jengo zaidi ya mara tatu ikiwa ni pamoja na kulifanyia tathmini.

“Wamefanya tathmini kuangalia maeneo ya kurekebisha, kubadili mabati, milango, madirisha na kuweka miundombinu ya kimahakama.

“Bajeti ya mwaka huu ndio jengo litafanyiwa ukarabati hivyo baada ya bajeti kuna kitu kitaendelea,”alisema.

Jengo hilo lilitolewa na mfadhili, Prosper Rweyendera kwa Serikali ya Wilaya ya Muleba tangu mwaka 2012.

Kata ya Ijumbi ina mahitaji makubwa ya huduma ya kimahakama kwa sababu kuna kata 11 zote zinategemea kupata huduma hiyo kutoka Mahakama ya Ishamba na Kashasha.

Akizungumzia Kituo cha Afya ambacho majengo matatu yalitolewa pia na mfadhili huyo, amesema kuna bajeti ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kuweka sawa miundombinu.

“Hiyo fedha haitatosha lakini tunasubiri ipatikane tuwafahamishe wananchi, kisha tufanye vikao vya kuweza kuchangia fedha kwa ajili ya kumalizia sehemu itakayokuwa imebakia.

Diwani wa kata ya Ijumbi, Wilbard Musirigi akizungumzia Kituo cha Afya amesema usajili unatarajia kufanyika ndani ya mwaka huu na ukarabati unatarajiwa kufanyika kuanzia Julai.

“Kliniki ya watoto na kina mama wajawazito inaendelea kufanyika katika majengo hayo,”alisema Diwani.

Alisema anaomba Waziri wa Afya atembelee katika Kituo hicho cha afya ili aweze kuona adha wanayopata wananchi kutafuta huduma.

“Mapato ya ndani yanatoka kwetu na malengo ya fedha hizo kuwekeza katika masuala ya maendeleo lakini hali haiko hivyo, tunaomba fedha zielekezwe kwenye maendeleo,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles