Renatha Kipaka, Bukoba
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wameshauri kuhimiza wananchi kujitoa katika kuchangia uanzishaji wa miradi ya maendeleo badala ya kutegemea Serikali pekee.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi​ wa halmashauri hiyo, Waziri Msafiri wakati akijibu​ taarifa za miradi ya maendeleo kwa mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu​ zilizokuwa zikiwasishwa kutoka kwenye kata mbalimbali zikigusia afya, barabara,elimu na ulinzi.
Msafiri amesema endapo madiwani wataongeza jitihada za kuhimiza wananchi kutenga maeneo na kuanzisha uwekaji wa maboma​ kama sehemu ya miradi ya maendeleo kwa kutegemea Serikali kukamilisha.
“Niwashauri madiwani​ kuweni na viwanja vya kujenga maboma kwenye maeneo ya wananchi pia waanzishe ili Serikali inapoombwa hela tuwe na maeneo ya kuonyesha jitihada zilizokwisha fanywa”amesema Msafiri
Diwani wa kata Kagondo Joram Ifunya, amesema katika kata hiyo kuna ukosefu wa zahanati ya kliniki ya mama na mtoto hali inayofanya usumbufu kwa jamii.
Amesema jamii inayoishi katika kata hiyo inatumia huduma ya kliniki Tembezi ambayo inamfuata alipo na kuna tatizo la utimilifunwa huduma hiyo.
Diwani wa kata Nshambya​ Meya wa Manispaa hiyo, Godson Rumanyika, amesema licha yakuwepo na uhaba wa zahanati kwa kila kata bado kuna tatizo la wahudumu wa afya ambao watahitajika kutoa huduma kwa jamii.
Amesema tayari kiasi cha sh.milioni 500 kimepangiwa kujenga hospitali ya Manispaa ya Bukoba licha ya kupambana na kuweka zahati kila kata