27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Wanamgambo wawauwa Wakristo wa Koptik Misri

Cairo, Misri

Wanamgambo wa itikadi kali za kiislamu jana wamewauwa watu saba na kuwajeruhi 19 walipoyashambulia mabasi matatu yaliyokuwa yamewabeba mahujaji wa Kikristo kuwapeleka katika monasteri moja ya jangwani kusini mwa mji mkuu wa Cairo.

Taarifa ya Kanisa la Orthodox la Koptik na Wizara ya Ndani imesema  watu 16 waliouawa katika  shambulio hilo walikuwa jamaa wa familia moja.

Wanamgambo wa eneo hilo  ambao wanahisiwa kufanya tukio hilo wenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) ambao wanaongoza harakati za kupambana na vikosi vya usalama katika Rasi ya Sinai, wamekiri  kuhusika na shambulizi hilo.

Naye   Rais  wa Misri Abdel Fattah el- Sisi amelaani shambulizi hilo huku akiapa kuendeleza vita dhidi ya ugaidi nchini humo.

Pia alituma salamu za rambirambi alipozungumza na Papa Tawadros II, kupitia simu ya mikono ambaye ndiye kiongozi wa kiroho wa Wakristo wa Orthodox nchini Misri, na mshirika wa karibu wa el Sissi.

Kwa upande wake kiongozi wa wakristo Papa  Tawadros amesema shambulizi hilo litawaongeza nguvu zaidi Wakristo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles