27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WANAKIJIJI MVOMERO WATEMBEA KILOMITA 20 KUPATA MATIBABU

Na Lilian Justice,

KIJIJI cha Kisimaguru  wilayani Mvomero katika Kata ya Hembeti kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa zahanati, imefahamika Hali hiyo husababisha wagonjwa kubebwa kwa machela zaidi ya kilomita 20 milimani kusaka huduma ya afya katika zahanati ya Hembeti.

Hayo yalielezwa jana na Diwani wa Kata ya Hembeti, Peter Mdidi katika mahojiano maalumu na Mtanzania.

Mdidi alisema wajawazito wanaotakiwa kujifungua hubebwa na machela na hivyo wengine kujikuta wakijifungulia njiani.

"Kutokana na changamoto ya umbali mrefu wa kufika katika zahanati ya Hembeti kunasababisha wajawazito kujifungulia njiani"alisema Mdidi.

Alisema kijiji kimeshajiwekea mkakati wa kujenga zahanati yake na hivi sasa wananchi wameanza kuchangia nguvu kazi.

Diwani huyo aliwaomba wadau na serikali wilayani humo kuchangia ujenzi huo uweze kukamilika kwa wakati.

"Tayari wananchi wameonyesha moyo wa kuchangia nguvu kazi katika ujenzi  huo hivyo tunawaomba wadau watuunge mkono kuwaondolea adha wananchi," alisema Mdidi.

Alisema Kijiji cha Kisimaguru kina jumla ya wakazi 800 aliwaomba wadau kutoingiza masuala ya siasa na badala yake waunge mkono juhudi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles