23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wanajeshi wauawa Chad

-N’Djamena

Maafisa wa jeshi wa ngazi za juu nchini Chad wameripotiwa kuuawa katika mapigano kati ya wanajeshi na kundi la waasi la Front for Change and Concord in Chad kaskazini mwa jimbo la Kanem nchini humo.

Mapigano hayo yameibuka kufuatiwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais nchini kuonyesha Rais Idriss Deby kuelekea kushinda muhula wake wa sita.

Nchi ya Marekani na Uingereza imewataka raia wake kuondoka nchini humo huku vikosi vya usalama vikiendelea kuweka hali ya amani.

Chama cha waasi cha Front for Change and Concord in Chad, ambacho kiko kusini mwa Libya, kilitoa ripoti ya kuteka kambi moja ya jeshi siku ya Ijumaa.

Jeshi la Chad limesema liliharibu msafara wa waasi siku Jumamosi ambao ulionekana ukikaribia mji wa Mao, karibu kilomita 220 maili 137 kaskazini mwa mji wa N’Djamena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles