31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

WANAJESHI WALIOASI IVORY COAST WAONDOKA BOUAKE

ABIDJAN, IVORY COAST


alassane-ouattaraWANAJESHI wa Ivory Coast wameondoka kwenye barabara za mji wa pili kwa ukubwa, Bouake, ambako walianza kuasi Ijumaa iliyopita wakitaka kuboreshwa kwa mishahara.

Hatua hiyo inafuatia tangazo la Rais Alassane Ouattara, kwamba amefikia makubaliano kuhusu pato na marupurupu yao.

Uasi huo ulitapakaa hadi sehemu nyingine za nchi, lakini wakazi wa miji iliyoathirika wanasema maisha yamerudi katika hali ya kawaida, na kwamba barabara na maduka yamefunguliwa.

Waziri wa Ulinzi, Alain Richard Donwahi ameachiwa huru baada ya kuzuiliwa kwa saa kadhaa na wanajeshi ambao walikuwa hawajaridhika na mapendekezo ya serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles