30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

Wanajeshi Kenya wadaiwa kujificha shambulio la al-Shabab

Lamu, Kenya

MAJESHI ya Kenya yamepinga vikali madai yaliyochapishwa katika gazeti la New York Times kwamba maofisa wake walijificha kwenye nyasi wakati wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab waliposhambulia kambi ya kijeshi ya Manda Bay.

Wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa katika shambulio hilo la Januari 5.

Kambi inayofahamika kama Camp Simba ambayo hutumiwa na vikosi vya Kenya na Marekani, ipo katika eneo la Hindi Magogoni pembezoni mwa kisiwa cha kitalii cha Lamu.

Taarifa ya New York Times ilidai kuwa utendaji kazi wa wanajeshi wa Kenya uliwatia hofu wenzao wa Marekani.

Pia ilisema kuwa wanamgambo wa Al-Shabab walinufaika na taarifa waliyopewa na Wakenya waliokuwa katika kambi hiyo.

Lakini msemaji wa majeshi ya Kenya, Kanali Paul Njuguna aliiambia BBC kuwa taarifa hiyo haikuegemea msingi wawote wa ukweli.

Aliongeza kuwa maelezo kuhusu shambulio hilo yatajulikana pale bodi iliyopewa jukumu la kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo itakapotoa ripoti yake.

“Taarifa hiyo haina msingi wowote. Uchunguzi unaendelea kwa mujibu wa wachunguzi, sio rasmi,” alisema Kanali Njuguna.

Gazeti la Kenya la Daily Nation pia lilimnukuu ofisa wa jeshi wa ngazi ya juu ambaye hakutajwa akisema; “Kambi ya Simba ni kituo cha kijeshi kinachotumiwa na Marekani kuendesha oparesheni ya kiusalama. Kinasimamiwa na kupewa ulinzi na Wamarekani.”

Vyanzo hivyo pia viliongeza: “Kilichofanyika katika kambi hiyo hadi sasa hakijafichuliwa, Marekani haijatoa taarifa kamili ni wanajeshi wangapi walikuwa katika kambi hiyo wakati wa shambulio hilo. Ni wao ndio wanaondesha mambo katika kambi hiyo.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles