24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanahisa MUCOBA Benki watakiwa kuinua benki yao

Na Raymond Minja, Mafinga

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini mkoani Iringa, Exaud Kigahe amewataka wanahisa wa Benki ya Mucoba kukubaliana na mabadiliko ya kukuza mtaji wao ili waweze kusonga mbele kibiashara.

Akizungumza kwenye katika Mkutano wa 21 wa Wanahisa wa Mucoba Kigahe alisema benki nyingi zimekuwa zikifa kutokana na kukosa ufanisi na koto kushirikiana na benk zenye uzoefu

Amesema kuwa ili benki ya Mucoba iweze kukuwa na kusonga mbele hawanabudi kukubalina mabadiloko kwa kushirikiana na banki zingine ili uwekezaji uwe wa kibiashara.

“Uwekezaji ambao umefanywa na benki ya watu wa Zanzibar (PBZ ) kuwekeza fedha nyingi ili kuhakikisha sekta ya biashara katika wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla unakuwa kupitia Mucoba ili kukuza mtaji wetu hayuwezi kujitenga kama tunataka kufika mbali hakunabudi kushirikiana,” amesema Kigahe.

Kigahe amesema kuwa Serikali inategemea maendeleo makubwa katika sekta binafsi ikiwa kuwawezesha wananchi kuwa na uwezo wa kufanyabiashara kwa kuwakopesha fedha ili waweze kufungua viwanda vya kuchakata mazao yao ya kilimo na sekta nyingine,

“Asilimia 80 ya wananchi wameajiriwa katika kilimo, masoko makubwa ya mazao yao yanategemea uwepo wa biashara pamoja na viwanda vya kuchakata mazao yao na kukuza uchumi kupitia sekta hii ya kilimo hivyo tunategemeana,” amesema.

Amesema uwepo wa uwekezaji huo wataweza kupata viwanda vikubwa ikiwa watapata uwezeshaji wa mikopo kutoka bank ya Mucoba ambapo kwa sasa wamepata nguvu kutoka bank ya PBZ.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Mafinga, Regnant Kivinge amesema viongozi wa benki hiyo ya wanapambana kuhakikisha Mucoba inasonga mbele na sio kubaki hapo ilipo.

Hata hivyo Kivinge aliwataka wanahisa kuendelea kuwekeza hisa zao katika benki hiyo kwani kwa sasa inafanya vizuri na mtaji wao umekuwa kutokana na vigezo vya benki kuu.

“Endeleeni kuweka hisa zenu kwenye benki yetu ya Mucoba kwa sasa inafanya vizuri ili mwisho wa siku tutaweza kupata faida ya kuwekeza hisa zetu katika benki yetu ya Mucoba na hatimaye kuvuna faida,” alisema Kivinge.

Aidha ameongeza kuwa benki hiyo kwa sasa ipo imara hivyo wanahisa wasiwe na mawazo ya kutoa hisa zao kutokana na changamoto ambazo zilijitokeza bali waongeze ili kukuza mtaji wao na mwisho wa siku waweze kufaidika

“Sisi wanahisa wa Mucoba tunajisikia faraja na kuwa na nguvu ya kusonga mbele kwa sababu tunapoana watu wa benki kuu na Watu wa Zanzibar (PBZ) tunaimani tutafanikiwa kwani benki yetu ipo imara kwa sasa,” amesema.

Akisoma taarifa kwa wajembe wa Mkutano huo Meneja wa benki hiyo, Philip Raymond amesema kuwa kutokana na gharama za uendeshaji kuongezeka kwa mwaka 2018 ukilinganisha mwaka 2017 wajumbe waliazimia bodi kuhakikisha inapunguza matumizi ili kuweza kuifanya benki kufanya vizuri zaidi ilicha ya changamoto walizozipitia hapo awali.

Philip amesema kuwa benki ya PBZ inawigo mkubwa kibiasha hivyo kushirikiana na bank ya Mucoba inaweza kupata fursa kubwa kujifunza na kukua kibiashara zaidi

Hata hivyo Meneja hiyo alisema kuwa benk hiyo imeendelea kuboresha huduma za mikopo kwa kupunguza riba ili kuongeza kiwango cha ukopeshaji.

Hata hivyo aliwataka wanahisa wa mucoba bank kuendelea kutumia bank hiyo kwa kuendelea kununua hiza ili benki hiyo iweze kufanya vyema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles