23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wanahabari waaswa kutumia kalamu zao vita dhidi ya dawa za kulevya

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutumia kalamu zao vyema katika vita dhidi ya dawa za kulevya inayoendelea nchini kwa kuwa kalamu ya mwandishi wa habari ni silaha yenye nguvu katika vita hiyo.

Hayo yalisemwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (DCEA), Gerald Kusaya wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wanahabari wa vyombo mbalimbali yaliyofanyika katika ofisi za Tume hiyo, jijini Dar es Salam jana.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Kamishna Kusaya aliwataka wanahabari kwenda kutoa elimu kwa jamii kutokana na mafunzo waliyoyapata huku akiongeza kuwa ana imani kuwa uwezo wa wanahabari na nguvu ya kalamu zao katika vita dhidi ya dawa za kulevya ni kubwa ikiwa watakuwa tayari kushiriki kikamilifu.

“Imani yangu ni kuwa mafunzo haya yatakuwa sehemu ya kichocheo cha kuelimisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya, tukishirikiana kila mmoja atajua tuna uhitaji wa kizazi kisicho na matumizi ya dawa za kulevya,” alisema Kamishna Kusaya.

Aliwataka waandishi na raia kushirikiana na Tume hiyo katika kutoa taarifa za biashara ya dawa za kulevya bila kuwa na hofu ya kutambulika kwani mamlaka hiyo ina watumishi wenye weledi na maadili ambao ukiwapa taarifa wataifanyia kazi bila kuleta madhara kwa watoa taarifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles