24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wanahabari Iringa watinga Hifadhi ya Ruaha kuchochea utalii

Na Raymond Minja, Iringa

Waandishi wa Habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari mkoani Iringa wametembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakiwa na lengo la kutangaza vivutio vya utali vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.

Akizungumza na wanahabari hao Juzi baada ya kumaliza ziara ndani ya hifadhi hiyo, Kamishina msaidizi wa hifadhi hiyo, Godwell Ole Meng’ataki amesema ushirikiano mkubwa kati ya sekta ya utalii na vyombo vya habari hapa nchini kutachochea ongezeko zaidi la watalii wa ndani na nje ya nchi.

Amesema ujio wa waandishi hao wa habari wapatao 40 waliotembelea hifadhi hiyo mategemeo yake ni kuwa ziara yao italeta tija katika sekta ya utalii kwa kuufahamisha umma kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vilivyopo katika hifadhi mbalimbali hapa nchini.

Ameongeza kuwa ziara hiyo ya wanahabari iwe chachu ya kuimarisha ushirikiano baina wahifadhi na wanahabari kwa lengo la kuibua mkakati wa pamoja katika kutangaza vivutio vilivyopo katika hifadhi za nchini Tanzania hususan vinavyopatikana katika hifadhi ya Ruaha ambayo ni ya pili kwa ukubwa katika ukanda wa Afrika.

Amesema wageni wanaotembelea hifadhi hiyo hupata fursa ya kujionea baadhi ya vivutio vya kipekee vilivyomo ndani ya ikiwemo simba wanaoishi kifamilia, ndege zaidi ya aina 574 na zaidi ya aina 1,650 za mimea inayopatikana katika hifadhi hiyo ya pekee hapa nchini.

Meng’ataki amefafanua zaidi kuwa katika hifadhi ya Ruaha kuna aina mbalimbali za utalii ukiwemo utalii wa kutembea kwa miguu, utalii wa usiku, utalii wa boti na utalii wa uvuvi wa samaki.

“Iwapo wanahabari mtatumia vyema kalamu zenu kutangaza utalii huu wa kipekee kikamilifu utachochea ongezeko la watalii katika hifadhi hii muhimu.

“Filamu ya Royal Tour iliyozinduliwa na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imekuwa na mchango mkubwa katika kuutangazia Ulimwengu juu ya vivutio vilivyopo hapa nchini,” amesema Meng’ataki.

Akimpongeza Rais Samia kwa kujitoa kwake katika kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii hapa nchini.

Meng’ataki amesema kitendo kilichofanywa na Rais kinapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania mzalendo mwenye nia njema na nchi yake hasa kwenye kukuza uchumi wa nchii yao.

Amina Rashini ni Afisa Uhifadhi Daraja la Kwanza.

Amina Rashini ni Afisa Uhifadhi Daraja la Kwanza katika hifadhi hiyo amesema kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) kwa mwezi Julai, 2022 ilipata watalii 2,232 ikiwa ni ongezeko la watalii 532 kutoka 1,700 walioitembelea kwa mwaka mzima wa 2021 kwenye hifadhi hiyo.

Amesema ongezeko hilo la watalii limetokana na filamu ya Royal Tour iliyosaidia kutangaza utalii ndani na nje nchi.

“Royal Tour imesaidia kutangaza hifadhi zetu kwa asilimia kubwa kwani baada ya Uviko 19 kupita watalii wameanza kurudi kwa kasi kwa watalii wa nje hawakuwepo, tulikuwa tunapata watalii wa ndani lakini sasa tunapata watalii wengi wa ndani na nje,” amesema Amina.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa Iringa, Frank Leonard alisema kuwa Waandishi wa habari Iringa wanatambua mchango wa utalii katika maendeleo ya taifa ndio Mana wakaamua kujitoa ili tutembelea Hifadhi hiyo na Hifadhi nyingine hapo baadaye.

Leonard amesema lengo la waandishi wa habari Iringa kutembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha ni kuhakikisha wanahamasisha sekta ya utalii hasa watalii wa ndani ili waweze kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya nchi yao.

Naye mwanahabari, Victor Meena alisema kuwa ziara iliyofanywa na wanahabari mkoa wa Iringa imekuwa na manufaa maa kubwa kwani licha ya wanahabari kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo utali lakini pia itasaidia kuchochea na kukuza utali hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles