23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wawili wafariki kwa kuangukiwa na mabomba ya maji Tabora

ALLAN VICENT

Watoto wawili wanaosoma katika Shule ya Msingi Kiyungi iliyopo katika
Manispaa ya Tabora wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na mabomba ya maji ya mradi wa ziwa Viktoria unaoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa huo.

Waliofariki ni mtoto wa darasa la tatu Paul Moses (9), na mwenzake Paul Clarance Chitopea (7) wa darasa la kwanza aliyefariki akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Tabora, Komanya Kitwala
amesema chanzo cha tukio hilo ni uangalizi mbovu wa mabomba hayo
ambayo yamelundikwa ovyo katika maeneo mbalimbali ya manispaa ikiwemo eneo hilo la shule.

Komanya amemwagiza Kamanda wa Polisi wilaya ya Tabora mjini (OCD)
kuanza uchunguzi wa tukio hilo haraka iwezekanavyo ili yeyote
atakayebainika kuzembea katika utendaji wake awajibishwe.

Aidha amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri ya manispaa hiyo, Bosco Ndunguru kutoa ushirikiano wa dhati kwa wafiwa wote ikiwemo kuhakikisha miili ya watoto hao inazikwa kokote watakapopendekeza wana ndugu ambapo ametoa Sh 150,000 kwa wafiwa.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, ACP Barnabas Mwakalukwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akibainisha chanzo chake kuwa ni watoto waliokuwa wakichezea mabomba hayo na kwa bahati mbaya yakawaangukia.

Ametoa wito kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari
ikiwemo kuonya watoto wao wasichezee mabomba hayo kwani ni mazito na likiwaangukia sio rahisi kupona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles