27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wasomea chini ya mwembe

mwembeNa Walter Mguluchuma-Katavi

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi  Kafisha wilayani Tanganyika, Mkoa wa  Katavi, wanalazimika kusomea masomo yao chini ya miti ya miembe kutokana  na shule hiyo yenye mikondo saba  kuwa na madarasa  mawili ya kusomea .

Hayo yalisemwa juzi na Diwani wa Kata ya Ikola, Philimoni Moro (CCM), alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazoikabili kata hiyo iliyoko mwambao mwa Ziwa Tanganyika.

Alisema shule  hiyo ina wanafunzi zaidi ya 600 na ina vyumba viwili vya  madarasa, huku  ikiwa na  mikondo ya kuanzia  darasa la kwanza  hadi  la  saba  pamoja na walimu saba.

Diwani  Moro  alisema  kipindi cha   mvua  za  masika  kimekaribia  kuanza,   hivyo  hajui  wanafunzi wa   shule  hiyo watakuwa  wanasomea wapi kwa kipindi hicho.

“Pamoja  na jitihada zilizofanywa  na  wananchi  za  kuchangia   madawati   katika shule hiyo, lakini wanavunjika moyo baada ya  kuona   madawati waliyochangia yakiwa yako nje yanapigwa na jua,” alisema.

Naye Mbunge wa Mpanda Vijijini,  Moshi Kakoso (CCM),  alikiri  kuwepo   kwa  tatizo la  upungufu  mkubwa  wa  vyumba  vya   madarasa

Alisema  tatizo hilo ni  la muda  mrefu ndiyo  maana    miaka   mine  iliyopita  yeye  kama  mbunge  aliweza  kutoa  msaada wa   madawati  kwenye  baadhi ya  shule  ambazo wanafunzi walikuwa wakisomea  chini  na pia  alichangia  vifaa vya ujenzi wa  majengo ya  madarasa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles