31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WALIVYOFUMBULIWA MACHO KUHUSU NDOA ZA UTOTONI

Na MWANDISHI WETU, aliyekuwa Zanzibar

DESEMBA mwaka jana, wadau wa Shirika lisilo la Kiserikali la Foundation for Civil Society (FCS), wawakilishi wa serikali na wadau wa maendeleo (DPs), walifanya ziara ya siku mbili visiwani Zanzibar ili kujifunza na kushauri asasi kadhaa visiwani humo.

Miongoni mwa wadau hao ni mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; kitengo cha asasi za kiraia na wawakilishi kutoka wadau watatu wa maendeleo wanaotoa fedha kwa FCS.

Wadau hao ni kutoka ubalozi wa Denmark; Jacqueline Ngoma kutoka  Shiriki la Maendeleo la Uswis (SDC) na Zabdiel Kimambo wa Ubalozi wa Uingereza kupitia idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID).

Bodi ya wakurugenzi ya FCS pia iliwakilishwa na wajumbe wawili akiwamo Mwenyekiti wake, Profesa Prosper Ngowi na Stephen Shayo.

FCS ilikuwa na wataalamu wake saba wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Wakili Francis Kiwanga.

Wengine ni Mkuu wa Idara ya Miradi, Francis Uhadi, Kitengo cha Ufuatiliaji, Guesturd Haule, Idara ya Kujenga Uwezo na Maendeleo, Edna Chilimo na Idara ya Uhuisishaji Biashara na Ushirikiano, Martha Olotu.

Ujumbe katika ziara hiyo ulitembelea asasi sita zikiwamo ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) upande wa Zanzibar, Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZAFELA), Chama cha Malezi Bora Tanzania (UMATI), Asasi ya Maendeleo ya Vijana ya SADEO na Mtandao wa Azaki Zanzibar (ONGOZA).

Katika ziara yao walitembelea mradi wa kutetea haki za wanawake katika masuala ya ardhi, Tamwa iliwaeleza wajumbe hao kuwa mradi huo ulioanza mwaka jana umeonesha mafanikio makubwa ya kuwafanya wanawake 40 kujiamini na kuelewa stahiki zao katika kushughulikia masuala ya ardhi kuliko hapo awali.

Mradi huo unatekelezwa katika wailaya za Kusini Unguja na  Kati Unguja. Tamwa iliendesha na mafunzo kuhusu haki za wanawake hasa zinazohusu masuala ya ardhi na kazi.

Asasi hiyo pia imetoa  machapisho kadhaa kufuatia sheria na sera kadhaa kwa kushirikiana na wadau mbalimbaluli ndani ya serikali na asasi nyingine.

Mapito ya sera kadhaa yameshawasilishwa kwenye vyombo husika ikiwamo Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Kamisheni ya Ardhi kwa utekelezaji.

Miongoni mwa mafanikio ya mradi huo wa Tamwa unaofadhiliwa kwa ruzuku kutoka FCS, ni uwezeshaji wa kushughulikia masuala 98 yanayohusu matatizo ya ardhi ambapo kati ya hayo 37 yamepatiwa ufumbuzi wa kudumu na mengine yakiwa mikononi mwa vyombo husika vya serikali.

Akizungumzia mafanikio hayo, Fatma Hassan wa shehia ya Kikungwi, anasema kabla ya mafunzo hayo wengi wao twalikuwa hawajui wakipata matatizo ya ardhi hasa ya kuporwa na wanaume au jamaa zao waende wapi lakini sasa wanajua.

Naye Tatu Shaabani wa Kijiji cha Kikungwi, anasema siku hizi waume zao wako mstari wa mbele kufuatilia haki za wanawake kutokana na uelewa wao si kama zamani ambapo walikuwa sehemu ya tatizo la wanawake kudhulumiwa ardhi na haki nyingine.

Wakiwa kwenye mtandao wa AZAKI Zanzibar (ANGOZA), ujumbe huo ulielezwa  jinsi mtandao huo ulivyowezesha wanachama wake kuyafahamu masuala ya uchambuzi wa bajeti na mfumo wa kufuatilia matumizi ya fedha za umma, maarufu kwa Kingereza PETS.

Hassan Khamis Juma, ni Mratibu wa mradi huo, anasema; "idadi kubwa ya wananchi  sasa wameanza kuulizia fedha za umma zinavyotumika na kutaka taarifa kila robo mwaka, jambo ambalo ni jema tofauti na ilivyokuwa awali."

Ujumbe wa wadau hao ulipotembelea Chama cha Wanasheria  Wanawake  Zanzibar (ZAFELA) ulielezwa jinsi mradi wa kuwajenga watoto kufahamu haki zao za ushiriki katika masuala yanayowahusu  ulivyofanikiwa.

Watoto wawili Abdulhamid Abdi, anayesoma Shule ya Mwanakerekwe F na Neema Said wa Shule ya Sekondari ya Haile Selassie, wanasema mradi huo umewajengea uthubutu na uwezo wa kuzungumza mbele ya  kadamnasi tofauti na awali.

"Sasa ninau uwezo wa kusimama mbele ya watu wakubwa zaidi yangu na kusema ninachotaka  bila ya woga wala kujisikia vibaya kama hapo mwanzo," anasema Abdulhamid.

Naye Neema anasema tangu wapate mafunzo hayo wamekuwa wakipaza sauti zao kuhusu masuala ya mimba za utotoni na kuolewa katika umri mdogo, mambo ambayo yanayofanyika zaidi Unguja.
Mkurugenzi wa ZAFELA, Jamillah Juma anasema kutokana na mradi huo wamegundua kuwa zile shutuma za awali kuwa wanaume wa dini ni vikwazo katika kubadili sheria za umri wa mtoto wa kike kuolewa  si za kweli.

Anasema dini ya Kiislamu inasema umri wa kuolewa ni miaka 21 hivyo hakuna mgongano wowote wa kimaslahi.

Msafara wa wadau hao pia ulifika Mangapwani, kilometa 20 kutoka Kaskazini Unguja kuwaona na kuongea na vijana katika asasi ya Safari Development Organization (SADEO) wanaotekeleza mradi wa kuunda mabaraza ya vijana kwa ufadhili wa ruzuku kutoka FCS.

Mbali na mafunzo mbalimbali kwa vijana 66, kusanyiko la vijana lilichagua wajumbe 33, watatu kutoka kila shehia kuunda baraza la vijana la Wilaya ya Kati Unguja.

Mtendaji wa SADEO, Mbaraka Nassoro Mbaraka anasema angalau sasa vijana wanaelewa uwapo wa Sera ya vijana na mfuko wa jimbo na jinsi ya kuchukua hatua ili kufahamu unavyofanya kazi.

"Tulikuwa hatujui lolote kuhusu uwapo wa sera ya vijana ya mwaka 2003 na sheria ya vijana ya mwaka huo huo inavyosisitiza umuhimu wa uundwaji wa mabaraza ya vijana," anasema Mbaraka.

Chama cha Malezi Bora  Tanzania (UMATI), walieleza na kusikiliza ushuhuda kutoka kwa wanufaika wa mradi huo kujenga uwezo wa jamii katika kuelewa sheria na masuala ya ardhi.

Tayari watu 400 walishapatiwa mafunzo kupitia mradi huo unaofadhiliwa na FCS kupitia mikutano ya hadhara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles