25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WA NIGERIA WASHAMBULIWA INDIA

UTTAR PRADESH, INDIA


WAZIRI wa Mambo ya Nje wa India, Sushma Swaraj, ameomba kufanyika kwa uchunguzi kufuatia tuhuma za kushambuliwa kwa Waafrika katika Jimbo la Uttar Pradesh.

Wanafunzi wanne kutoka Nigeria wanauguza majeraha baada ya kushambuliwa.

Msichana raia wa Nigeria, ameripotiwa kutekwa huku Waafrika wengine wakishambuliwa wakati wa maandamano ya kupinga kifo cha mvulana mmoja raia wa India katika mji wa Noida uliokumbwa na ghasia.

Inahofiwa mvulana huyo alipewa dawa za kulevya kupita kiasi.

Waafrika ndio wanaotuhumiwa kwa uuzaji dawa hizo, na raia watano wa Nigeria walikamatwa wakihusishwa na tukio hilo kabla ya kuachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi.

Aidha raia wa Nigeria walishambuliwa siku ya Ijumaa katika mji huo kwa tuhuma za kula watu.

Sharawaj alisema waziri mkuu wa jimbo la Uttar Pradesh amemhakikishia uchunguzi huru utafanywa kuhusu matukio ya kushambuliwa kwa wanafunzi hao.

Kwa mujibu wa taarifa kwenye vyombo vya habari, polisi wamewakamata watu watano.

Kulishuhudiwa mashambulio kadhaa dhidi ya Waafrika mwaka jana katika mji mkuu wa Delhi.

Baadhi ya ofisi za kibalozi za mataifa ya Afrika ziliilalamikia Serikali ya India baada ya wanafunzi kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushambuliwa katika miji mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles