25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WA KIMATAIFA WANAVYOHOFIA MITANDAO

MITANDAO ya kijamii imekuwa nguzo muhimu kwa wanafunzi wa kimataifa hasa katika kubadilisha mfumo wa maisha wa tamaduni tofauti hasa nchini Marekani.

Wanafunzi wa kimataifa hutumia mitandao ya kijamii kuwaunganisha na familia zao katika nchi wanakotoka.

Kwa mujibu wa utafiti mpya uliyofanywa na Chuo Kikuu cha Kansas nchini Marekani umegundua huwa wanafunzi wa kimataifa wanaotumia mitandao ya kijamii inawasaidia kuwa na mawazo chanya ikilinganisha na msaada wa kijamii wanaopokea katika kampasi ya chuo.

Profesa Msaidizi wa Uandishi wa Chuo Kikuu cha Kansas, Hyunjin Seo anasema utafiti umebanisha kwamba matumizi ya mitandao ya kijamii yanabadilisha maisha ya wanafunzi wa kimataifa katika vyuo vikuu.

“Mitandao ya kijamii inawasaidia wanafunzi kuwasiliana na ndugu nchi wanakotoka kwa kudumisha mawasiliano,” anasema Seo.

Anasema waligundua matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wanafunzi kunaweza kuchangia maendelo yao kwa sababu wanajisikia kuwa wapo karibu na ndugu na marafiki.

Wanafunzi wa kimataifa hutumia njia ya mitandao mbalimbali ya kijamii hususani  mtandao maarufu duniani wa Facebook, pamoja na mitandao mingine kama Twitter, Instagram, Snapchat, YouTube, WhatsApp na Wechat ambao ni maarufu sana nchini China.

Matumizi ya mitandao ya kijamii inaonekana kuwa mchango mkubwa wa kubadilisha maisha ya wanafunzi katika jamii hasa wakiwa nchi za kigeni.

Hata hivyo, utafiti huo ulibainisha kuwa wanafunzi wa kimataifa kwa kiasi kikubwa hawatumii mitandao ya kijamii katika kujadili matatizo binafsi kwenye mitandao kwa sababu za kitamaduni.

Wanafunzi hao wanasema hawataki kujadili matatizo ya uhusiano kwenye mitandao kwa sababu wanaogopa wazazi wataona na kuleta matatizo  ya kifamilia.

Aidha wanafunzi wengi wanasema mitandao ya kijamii imewasaidia kuunganisha marafiki wanaosoma nchi mbalimbali ikiwamo Marekani.

Pia wanasema mitandao ya kijamii imekuwa msaada mkubwa kwa kuwaunganisha na tamaduni tofauti za kwao.

Kwa upande mwingine, utafiti huo ulibainisha kuwa upweke unaweza kuwa chanzo kikuu cha matatizo ya msongamano wa mawazo kwa wanafunzi kitu ambacho kinaweza kusababisha matatizo ya kitaaluma.

Seo anasema katika kusaidia kupunguza upweke, mitandao ya kijamii huwa msaada mkubwa kwa  wanafunzi kama huo.

Vyuo vikuu vya kimataifa vinaweza kutumia mitandao ya kijamii kama njia ya kuwafikia na kuwasaidia wanafunzi wa kimataifa.

"Utafiti huu unaonyesha kuwa mitandao ya kijamii ni jukwaa muhimu kwa wanafunzi wa kimataifa kuzoea maisha ya chuo," anasema Seo na kuongeza:

"Vyuo vinaweza kutumia mitandao katika kuwahusisha wanafunzi wa kimataifa kwenye majukwaa ya kijamii au kuunganisha waliohitimu.

Taasisi za elimu ya juu mara nyingi wanajaribu kutumia teknolojia kuwasiliana na wanafunzi. Kwa upande wanafunzi wamekuwa wakizoea teknolojia mpya.

Vyuo vikuu vinapaswa kuelewa maeneo ambayo wanafunzi wanapata mawasiliano na wanzao au kupata taarifa ya vyuo bora uwezo, vyuo vinatakiwa kuwepo na kushiriki wanafunzi katika kuwasaidia kunufaika kupitia mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles