30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WA KIKE WAPIMWA UJAUZITO

Na Samwel Mwanga,

WAZAZI wa wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Maswa   wameishauri idara ya elimu kwa kuanzisha kuwapima ujauzito wanafunzi wa kike.

Wanafunzi hao ni  kuanzia darasa la tatu hadi kidato cha sita   lengo likiwa ni kudhibiti vitendo vilivyokithiri vya wanafunzi hao kupata ujauzito.

Kwa mujibu wa wazazi hao,  njia pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuanza utaratibu wa kuwapima ujauzito wanafunzi hao wanapokuwapo shuleni.

Walisema miononi mwa matatizo makubwa yanayosababisha kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani  ni pamoja na wanafunzi wa kike kupatiwa ujauzito wakiwa shuleni na hivyo kukatisha masomo.

“Katika wilaya yetu tuna tatizo kubwa la wanafunzi wetu wa kike hasa wa shule za msingi kutomaliza masomo yao kwa kupatiwa ujauzito.

“Suala hili linachangia kwa kiasi kikubwa kushuka  kiwango cha elimu sasa ufike wakati wa kukomesha suala hili,” alisema Angelina Martine.

Walisema  dara ya elimu ikishirikiana na idara ya afya wilayani humo iliamua kuchukua hatua  hiyo   la kudhibiti vitendo vya ngono kwa wanafunzi   kwa vile  wengi  wao ni wenye umri wa kati ya miaka minane hadi 16.

“Unajua wanafunzi wa madarasa hayo wameanza kuwa na umri mkubwa maana ilishawahi kutokea   Wilaya ya Bukombe mkoani Geita mwanafunzi wa darasa la tatu akiwa mjamzito.

“Lengo ni kudhibiti vitendo vya ngono kwa wanafunzi  shuleni na wakiona upimaji unafanyika wengi wao wataogopa na kujihusisha na vitendo hivyo,” alisema Rhoda John.

Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Maswa,Simon Bujimu, alisema  wazo hilo ni zuri na utaratibu huo ulishawahi kutumia na   kuwabaini wanafunzi   wajawazito.

Alisema  kwa sasa zitaongezwa nguvu  kupambana na tatizo hilo.

Aliwaomba wazazi nao kukaa chini na watoto wao na kuwaeleza madhara ya kupata ujauzito wakiwa bado masomoni.

Takwimu zinaonyesha katika kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya wanafunzi 50 wa kike wa shule za msingi na sekondari wilayani  walilazimika kuacha masomo kutokana na  ujauzito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles