31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi Shule ya wenye mahitaji maalum wamwangukia Samia

Na Ramadhan Hassan,Chamwino

SHULE ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Wasioona ya  Buigiri Wilayani Chamwino mkoani Dodoma  imemwangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan awasaidie Sh milioni 8 kwa mwezi kwa ajili ya kuendesha kituo hicho.

Hayo yameelezwa Mei 12 mwaka huu na  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,Godfrey Daudi wakati akipokea msaada wa chakula,mafuta,sabuni,juice,taulo za kike  na sare za shule zilizotolewa na Saccos ya Mfuko  wa Hifadhi ya Jamii  kwa watumishi wa Umma (PSSSF).

Mwalimu huyo amesema changamoto wanazokabiliwa nazo  ni pamoja na bajeti kutokukidhi kwa sababu matumizi wanayotumia  kwa mwezi ni shilingi  milioni tatu kwa ajili ya bili za umeme,maji,chakula  na matibabu kwa wanafunzi.

Hata hivyo, anasema mahitaji yao  kwa mwezi ni shilingi  milioni 8 hivyo wanamuomba Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan awasaidie ili waweze kuwasaidia wanafunzi waliopo katika shule hiyo.

“Kwa kushirikiana na Serikali yetu inayoongozwa na mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan ambaye tunamuombea usiku na mchana kwa manufaa ya Taifa letu sisi bajeti yetu ni shilingi milioni 8 kwa mwezi  na tunamuomba mama yetu aliangalie hili tunajua atafanya,”amesema.

Amesema shule hiyo ina wanafunzi 119 ambao ni wasiiona kabisa,wenye uoni hafifu,wenye ulemavu wa ngozi na wa kawaida kwa ajili ya sera ya elimu jumuishi.

Mwalimu huyo aliishukuru PSSSF Saccos kwa misaada waliyoitoa huku akizitaka Taasisi na Mashirika mengine ya umma kuiga mfano wa mfuko huo.

“Kwanza niwashukuru kwa mamna wanavyotoa sapoti niwaombe waongeze nguvu kwa sababu namna hawa walivyo ni mapenzi ya mungu na hakuna walichomkosea mungu.Natamani sana suala la bajeti na kwa hilo nikuishukuru Serikali kwa sababu inaunga mkono inafanya mambo makubwa sana kwenye hii shule kwa sababu inafanya ujenzi wa bweni lenye thamani ya shilingi milioni 80,”amesema.

Kwa upande wake,Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,amesema wamefika katika shule  hiyo  kutokana na wajibu wa Saccos yao kuchangia jamii  na  kusaidia watu wenye mahitaji maalum hivyo wamewapatia vyakula,mafuta, sabuni,juice za watoto,sare za shule taulo za watoto wa kike zenye thamani ya shilingi milioni 2.

Amesema ni mara yao ya kwanza kufanya jambo hilo ambapo amedai kwa sasa utakuwa ni utaratibu wao kila mwaka kusaidia watoto wenye mahitaji maalum katika vituo mbalimbali.

“Hapa ndio tumeanza mara zote hatutaliacha kabisa na sio lazima kiwe kituo hichi tu na  siku nyingine tutaangalia kitu kingine chenye uhitaji.Jambo hili,linatakiwa lifanyike kila mwaka lakini Saccos yetu bado ndogo lakini kwa mwaka huu ndio tumetoa,”amesema.

Amesema jukumu la kutunza watoto wenye mahitaji  ni la kila mmoja hivyo jamii inapaswa kupeleka kidogo kidogo ili kuwapa furaha na kuwafanya wasahau matatizo yao.

“Tunaiambia Serikali jukumu la kutunza watoto kama hawa ni la kila jamii ambayo inauwezo kwa sababu wao wenyewe hawajajitosheleza mahitaji yao lakini kila jamii ikilea kidogo kidogo kwa furaha bila kukumbuka matatizo yao walioyonayo,”amesema.

Naye, Dada Mkuu wa shule hiyo,Lucy Michael ameiomba jamii izidi kuwatembelea watu wenye ulemavu na wenye  mahitaji maalum huku akidai ndoto yake ni kuwa mtangazaji katika siku za baadae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles