WANAFUNZI KUMI WAPEWA MIMBA NJOMBE

2
1487
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri,
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri,

Na Elizabeth Kilindi – Njombe

ZAIDI ya wanafunzi kumi wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, wamedaiwa kushindwa kuendelea na masomo mara baada ya kupata mimba shuleni kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2016 hadi Juni 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, idadi kubwa ya wanafunzi wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ngono hali ambayo inasababisha baadhi yao kupata mimba wakiwa masomoni na kukatiza ndoto zao.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo, Avelino Chaula, alisema jamii na Serikali zinatakiwa kufanya kila jitihada kuzuia matukio hayo kwani yamekuwa yakichangia uwepo wa watoto wa mitaani na kuongezeka kwa umasikini katika familia.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri, alisema watoto hawatakiwi kuzaa wakiwa shule kwani taifa litashindwa kuendelea kutokana na kujadili swala hilo mara kwa mara.

Kwa upande wao, madiwani walisema pamoja na wananchi kujitahidi kupambana na vitendo hivyo, lakini Jeshi la Polisi limekuwa likiwakatisha tamaa ya kukabiliana na watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi kwani limekuwa likiwaachia  kwa madai ya uchunguzi unaendelea na kusababisha kupata mwanya wa kutoroka.

“Wananchi tunashiriki vizuri katika kuwakamata wahalifu wanaowapa wanafunzi mimba na kuwapeleka polisi, lakini hatuoni mwisho wa kesi hizo.

“Hii hali inatukatisha tamaa, ukiangalia kama vile polisi wanahusika kutorosha watuhumiwa, mimi mwenyewe nimeshashiriki kumkata kijana mmoja na kumpeleka polisi, lakini baada ya muda akatoroka,” alisema Diwani wa Kata ya Kidegembie, Julias Salingwa.

2 COMMENTS

  1. Ee tunspeleka maendeleo kwanza nyumbani wanakotoka maraisi. Tumesnzia Chalinze, tupo chato sasa na rsisi wa awamu ya tatu akiunga mkono. Kibiti ndo hivyo. Watoto na wasichana wenye ujauzito wanaohitaji pesa za kuwaendeleza kielimu na serikali hakuna ruksa,maraisi walioshindwa kutetea , kulinda mali za watsnzania hakuna kuguswa, na wanapelekewa miradi mikubwa vijijini kwao.je, lipi la muhimu zaifi, elimu kwa maskini au?
    Tufikirie sana namna gsni utajiri wa nchi maskini hawamjali.wenye kupewa madaraka nchini, je tunatumia madaraka yetu vizuri. Inaleta picha gani kujenga nyumbani kwetu kwanza badala ya kuangalia umuhimu na matumizi bora ya mali za umma kwa nchi nzima.Tunatumbua nini.majipu.mengine tunayakumbatia. Hongera kwa utumbuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here