27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi hewa 65,000 wagundulika nchini

Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene
Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene

Na RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WANAFUNZI hewa 65,198 wamegundulika katika shule za msingi na sekondari nchini.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Simbachawene, kitendo cha kuwagundua wanafunzi hao, kimeokoa Sh milioni 931.3 ambazo zilitarajiwa kupelekwa shuleni kuwahudumia wanafunzi hao katika mwaka 2016/ 2017.

“Kati ya wanafunzi hao, wale wa shule za msingi ni 52,783 na wa sekondari ni 12,415.

“Kwa ujumla, uhakiki huo ulifanyika mikoa yote nchini kufuatia agizo la Serikali kwa makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara.

“Shilingi bilioni 27 zimekuwa zikipelekwa kila mwezi kama ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka kwa ajili ya wakuu wa shule na walimu wakuu, lakini baadhi ya walimu waliamua
kuongeza idadi ya wanafunzi ili wapate fedha zaidi.

“Kwa kuwa hilo tumelijua, hatua za kinidhamu zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wote waliosababisha uwepo wa wanafunzi hewa na Tamisemi inaendelea kuhakiki takwimu zilizowasilishwa,” alisema Simbachawene.
Kutokana na hali hiyo, waziri huyo alisema Serikali haitegemei tena kuwapo kwa wanafunzi hewa kwa makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za mitaa na wakuu wa shule, wanatakiwa kudhibiti suala hilo.

Aliitaja mikoa inayoongoza kuwa na wanafunzi hao kuwa ni Tabora (12,112), Ruvuma (7,743), Mwanza (7,349), Dar es Salaam (4,096), Kagera
(4,763), Rukwa (4,054), Singida (3,239), Kilimanjaro (2,594), Kigoma (2,323), Njombe (2,307), Simiyu (2,081) na Arusha (1,923).
Mikoa mingine ni Mara (1,855), Tanga (1,378), Geita (1,281) Morogoro (1,172), Mtwara (882), Mbeya (786), Shinyanga (695), Songwe (512), Manyara (330), Dodoma (284), Lindi (281), Pwani (187), Iringa (161) na Katavi (0).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles