33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 80 warejea shule Muleba

Na Renatha Kipaka, Muleba

Wanafunzi 80 warejea shule wilayani Muleba mkoani Kagera katika kipindi cha mwaka 2020/21 baada ya kufanyika kwa oparesheni ya kurejesha wanafunzi shuleni iliyosimamiwa na viongozi wa wilaya hiyo.

Hayo yamebainishwa juzi na Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Muleba, Mwl. Seveline Musyangi alipotembelewa na Waandishi wa Habari ofisini kwake kwa lengo la kufahamu namna wanavyopambana kudhibiti utoro shuleni.

Musyangi amesema kuwa tayari ndani ya mwaka huu wanafunzi hao waliokuwa watoro wamesajiriwa kufanya mtihani wa darasa la saba na kwamba wavulana ni 43 na wasichana 37.

Ametaja chanzo cha utoro kuwa ni umbali wa shule na utoro wa rejareja unaosababisha wanafunzi wasifanye mitihani ya kupanda madarasa.

Ameongeza kuwa halmashauri hiyo imeendelea kufuatilia mahudhurio yao toka wamesajiliwa kwa kushirikiana na walimu wakuu wa shule ili kuhakikisha wanafanya mtihani na kwamba kila wiki wamekuwa wakifuatilia shuleni mahudhurio ya wanafunzi hao.

Ametoa wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao kwa kuwasikiliza na kuwapa nafasi ya kuongea ili kujua changamoto wanazopitia.

“Nitumie nafasi hii kusema kuwa mtoto wako ni mtoto wetu jamii nayo inayo nafasi ukiona mambo hayaendi vizuri kwa mtoto wako, chukua hatua usione mtoto anafanyiwa ukatili ukanyamanza hapo tutakuwa tunatengeneza Taifa la namna gani, hivyo tuchukue hatua kwa ajili ya ulinzi wa mtoto anapokuwa shuleni hata nyumba,” amesema.

Kwa upande wake mzazi, Joseph Kamugisha ambaye ni baba wa watoto watano na mkazi wa Kata ya Katoke Kijiji cha Kimbugu amesema kuwa changamoto inayosababisha utoro kwa wanafunzi, kwanza ni ufuatiliaji wa wazazi kwa watoto wao ni mdogo, hivyo unachangia watoto elimu kuichukulia kawaida kiasi kwamba mtoto anaaga kwenda shule kumbe yuko vichakani na wakati mwingine watoto wa kike kuangukia kwenye mikono ya uharibifu.

Mzee Joseph Kamugisha ameongeza kuwa watoto wengi wanakimbilia kwenye uvuvi kwa kisingizo cha kutafuta pesa na kuacha mambo ya msingi kama elimu na mambo mengi yanayohusu ndoto za malengo yao.

“Mimi mzazi nitumie nafasi hii kuwaomba wazazi wenzangu kutoa ushirikiano wa karibu kwa watoto wetu, tusiwatelekeze tunapo wapeleka shuleni nasi tuhusike kwa karibu kufuatilia maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wawapo shuleni ili kuzungumza na walimu wao na kujua maendeleo yao kielimu,” amesema Kamugisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles