Wanafunzi 30 wapeta kinyang’anyiro wazo bora la biashara

0
1163

Christina Gauluhanga

Wanafunzi 30 kutoka katika shule sita za sekondari jijini Dar es Salam wanaosema mkondo wa Sayansi, wamefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha wazo bora la biashara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Desemba 5, Mlezi wa Taasisi ya Fizikia nchini (IOP), Dk. Askwar Hilonga amesema mchakato huo umechukua mwaka mzima ukizishirikisha shule 40.

Amesema lengo ni kuwajengea uwezo na kukuza mawazo yao kuweza kuingia katika biashara.

“Kwa watakaoshinda wataingizwa katika mafunzo ya vitendo ambayo hadi wanamaliza mafunzo hayo wanakuwa wamebobea kusajili kampuni ya biashara,” amesema Hilonga.

Amesema sababu ya kuchagua wanafunzi wa Sayansi ni kwa sababu wanasayansi wengi kufanya tafiti nyingi zenye kusaidia jamii lakini matokeo yake zinaishia kwenye makaratasi.

“Kwa kuwajengea uwezo tafiti hizo zitajibu changamoto za jamii na kuwapatia ajira wanafunzi hao,” amesema Hilonga.

Amezitaja Shule za sekondari zilizoingia sita bora ni Baobab Girls and Boys, Chang’ombe, Tusiime, Shamsiya na Jangwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here