20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Wanafunzi 270 wasomea chini ya mti Musoma

Ahmed Makongo -Musoma

ZAIDI ya wanafunzi 270 wa Shule ya Msingi Wanyere B, Kata ya Suguti, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara, wanasoma wakiwa chini ya mti kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

MTANZANIA ilizungumza na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Peter James ambaye alisema kuwa wanafunzi hao wanasoma wakiwa katika hali hiyo kutokana na upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa.

James alisema kuwa kutokana na hali hiyo walimu wamekuwa wakipata changamoto ya ufundishaji na kwamba pia uelewa kwa wanafunzi hao unakuwa ni mgumu.

“Ni kweli wanafunzi wa madarasa matatu yenye jumla ya watoto 274 katika shule yetu wanasomea nje kwenye mti kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa,” alisema James.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Wanyere, Thomas Musiba, alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walihamasishwa na kuanza kuchangia fedha ili kuiondoa changamoto hiyo.

Musiba alisema kuwa hata hivyo fedha walizochanga wananchi kwa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, zimechakachuliwa na viongozi waliokuwa madarakani na kusababisha ujenzi huo kutokufanyika.

Alisema kuwa wananchi hao walichanga fedha hizo kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 kutokana na agizo la Mkuu wa Wilaya, Dk. Vicent Naano, ili kuwanusuru wanafunzi hao waweze kupata mahali pa kusomea.

“Wananchi walianza kuchanga fedha hizo tangu mwaka 2017 hadi mwaka 2019 na kwa kila kaya kuchangia kiasi cha Sh 15,000, ikiwa ni pamoja na waliochelewa kuchanga mchango huo walipigwa faini ya Sh 10,000 kwa kila kaya,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles