23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 15,942 waingia mitini Kagera

*Utoro, ukosefu wa hamasa vyatajwa

Na Renatha Kipaka, Kagera

Jumla ya Wanafunzi 15,942 mkoani Kagera hawakuhitimu kidato cha nne kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na sababau mbalimbali zilizopelekea kuwa na utoro wa moja kwa moja.

Afisa Elimu Mkoa wa Kagera, Khalifa Shemahonge wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 24, mwaka huu, Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera, Khalifa Shemahonge amesema, mkoa umeanza kubaini wanafunzi ambao walijiunga na kidato cha kwanza lakini hawakuweza kuhitimu kidato cha nne na kuanagalia sababu zinazosababisha.

“Niseme tu idadi hiyo inaanzia mwaka 2019 hadi 2021 ambapo wavulana ni 7,547 na wasichana ni 8,395. Ukiangalia kwa kila mwaka, 2019 idadi ilikuwa 4,416, mwaka 2020 ilikuwa 5,199 na mwaka jana ilikuwa 6,327,” amesema Shemahonge.

Aidha, amesema kuwa baada ya ufuatiliaji sababu zilionekana kuwa ni utoro na kwenda kufanya kazi maeneo mbalimbali huku mimba pia zikitajwa kwa wanafunzi wa kike.

Amesema kuondoa hali hiyo shuleni hatua ya kuanza kuweka mbinu bora na rafiki kwa wanafunzi kupenda kuendelea na masomo shuleni zitafanywa kwa ushirikiano wa walimu na uongozi wa mitaa, vijiji na kata.

“Sasa tupo kwenye utaratibu wa kuangalia nijinsi gani tutafanya ili kuanzisha utaratibu wa kuwapatia wanafunzi chakura pamoja na michezo ili kuongeza hamasa kwa watoto hiyo itasaidia kupunguza utoro,”amesema Shemahonge.

Asikofu Dayosisi ya Kasikazini Magharibi la KKKT, Abednego Keshomshara.

Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Bukoba, Kagera, Abednego Keshomshahara amesema kwa kutambua matatizo ya mimba kwa watoto wa kike majumbani wamesaidia kutoa semina za ujasirimali.

Alisema watoto wanaopata mimba ni wale wa kuanzia umri wa miaka14 hadi 17 nakwamba sababu ni mazingira magumu wanayoishi wengi wao ikiwamo familia duni.

“Wapo watoto waliozalia majumbani lakini walikuwa na ndoto za kufika sehemu ambayo ingewatoa kwenya hali ya umaskini na kuwasaidia kutoka katika hali ya utegemezi kutokana na utoto na changamoto za maisha mtoto anazaa mtoto mwenzie,” amesema Keshomshahara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles