Wanachama TPSF kuendelea kupambana na corona

0
463

Mwandishi Wetu -Dar es salaam

TAASISI ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imelihakikishia taifa kwamba wanachama wake wataendelea kwa nguvu zoke kukomaza ubunifu katika kupambana na ugonjwa wa corona kwa kuwa Tanzania imeruhusu uzalishaji uendelee mashambani, viwandani na maofisini.

Akizungumza mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula alisema kuwa taasisi yake itaendelea kuunga mkono Serikali  katika  jitihada zake za  kupambana na janga la corona.

“Tunaendelea kuipongeza Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zinaoendelea kuchukuliwa. 

“TPSF kwa kushirikiana na wadau wetu tutakuwa bega kwa bega katika kuunga mkono jitihada hizo mpaka pale tutakapohakikisha kasi ya maambukizi inapungua na kupotea kabisa,’’ alisema Angelina ambaye taasisi yake ilikabidhi msaada wa Sh bilioni 2.1 kwa Serikali.

Angelina aliishukuru Serikali kwa kuruhusu kazi ziendelee katika maeneo yote ya uchumi wa taifa.

“Kutofunga shughuli za uchumi kumechochea ubunifu kwa wadau wa sekta binafsi. Hivi sasa wamejikita katika uzalishaji wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya corona ikiwemo barakoa, sanitizer, ndoo na  matanki ya kuimarisha tabia ya watu kunawa mikono. 

“Ubunifu wa aina hii  umelinda ajira za Watanzania na kuimarisha uchumi wa nchi katika kipindi hiki cha janga,’’ alisema Angelina. 

Alisema kuwa TPSF imepokea wito chanya wa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wa kuwataka wanachama wa taasisi hiyo kutengeneza kila kinachowezekana kuwakinga wananchi na virusi vya corona, ikiwemo  vifaa vya kinga na sanitizer.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here