23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

WANACHAMA NCCR-MAGEUZI WAMTAKA MBATIA KUJIUZULU

BAADHI ya wanachama wa NCCR-Mageuzi wamemtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na Katibu Mkuu wa chama hicho, Martin Danda kujiuzulu ndani ya siku tatu kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwamo ubadhirifu wa fedha na kutaka kukiua chama hicho.

Mbatia anadaiwa kuuza mali za chama zikiwamo nyumba mbili zilizoko jijini Dar es Salaam eneo la Bunju B, moja iliyoko Tarime mkoani Mara na shamba la ekari 56 lililoko Bagamoyo mkoani Pwani.

Faustine Sungura mmoja wa wanachama wa chama hicho, amesema mbali na kuuza nyumba pia Mbatia ana mkakati maalumu wa kuiua NCCR na kuhamia Chadema ambako ameahidiwa ukatibu Mkuu.

“Hivi sasa kuna mkakati wa kuuza nyumba nyingine za chama zilizopo mkoani Rukwa na Katavi na mauzo yatakabidhiwa kwake kwa madai kuwa anakidai chama fedha alizokikopesha wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, tunatoa tahadhari kwa watu kutonunua nyumba hizo kwani watapata hasara isiyotibika,” alisema.

Pamoja na mambo mengine Sungura amesema viongozi hao wasipojiuzulu atawafungulia mashtaka mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles