30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Wan-Bissaka kuikosa ‘pre-season’ United

MANCHESTER, ENGLAND 

BEKI wa timu ya Manchester United, Aaron Wan-Bissaka, yupo hatarini kuyakosa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England akiwa na kikosi hicho baada ya kupinga utaratibu wa kujikinga na virusi vya corona.

Wachezaji wa timu hiyo walipewa utaratibu jinsi ya kujikinga na sehemu za mikusanyiko ya watu ambayo inaweza kusabisha kupata maambukizi ya virusi vya corona ikiwa pamoja na kutosafiri baadhi za nchi.

Lakini mchezaji huyo alionekana akiwa nchini Dubai kwa ajili ya mapumziko jambo ambalo linawapa wasiwasi viongozi wa timu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, mchezaji huyo anatakiwa kukaa karantini kwa siku 14 kabla ya kuungana na wachezaji wenzake ambao kwa sasa wanataka kufanya maandalizi ya msimu mpya.

Manchester United wanatarajia kuanza maandalizi hayo mapema wiki ijayo, hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, hatokuwa kwenye kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.

Hata hivyo, Manchester United wamedai mchezaji huyo akiwasili mwishoni mwa wiki hii atafanyiwa vipimo kabla ya kwenda karantini.

Mtandao wa Sportsmail, unaamini kuwa, mchezaji huyo alikwenda nchini Dubai sio kwa ajili ya starehe, ila alikwenda kwa ajili ya kujiweka sawa na msimu mpya wa Ligi kutokana na picha zinazosambaa akiwa anafanya mazoezi kwenye fukwe mbalimbali.

Michuano ya Ligi Kuu nchini England msimu huu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu.

Kwa upande mwingine, mchezaji huyo raia wa nchini Uingereza ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa chini ya kocha Gareth Southgate kwa ajili ya maandalizi ya Nations League dhidi ya Iceland na Denmark.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles