23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki wa viwanda wavunja ukimya umeme wa Tanesco

Bakari Kimwanga, Arusha

Wateja wakubwa wanaohudumiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), katika Mkoa wa Arusha wamepongeza kazi inayofanywa na shirika hilo katika kuboresa huduma zake ikiwamo kupatikana kwa umeme wa uhakika wakati wote jambo linalosaidia kuimarisha uzalishaji kwenye viwanda vyao.

Hayo wameyasema jana mjini hapa katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari ya kutembelea shughuli za Tanesco,  ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Sailesh Pandit amesema kuimarika kwa huduma za umeme sasa umekifanya kiwanda chake kiweze kutumia megawati 7 kila mwezi na kulipa bili kati ya Sh milioni 500 hadi 600 kwa mwezi kutokana na uzalishaji wake.

Wengine waliosifu huduma hizo ni  viwanda vya A to Z kilichoko eneo la Kisongo na kile cha kutengeneza nguo cha Sunflag, kilichoko Themi.

Pandit amesema kuimarika kwa huduma za Tanesco zimemfanya ashiwishike kufungua viwanda vingine vitatu kimoja kikiwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

 “Zamani tulikuwa na shida sana miaka miwili mitatu iliyopita, power cut (kukatika kwa umeme), sasa hivi hamna ni mara chache sasa labda ikitokea kwenye gridi ya taifa hapo hatuna ha kufanya, lakini sasa hivi hatuna tatizo la umeme kabisa,” amesema Pandit.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles