26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wamiliki wa viwanda watakiwa kupambana na bidhaa bandia

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Edwin Mhede, amewataka wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kushirikikiana na Tume ya Ushindani (FCC) kupambana na bandia kwa sababu wanayo nafasi kubwa ya kuelewa pale bidhaa zao zinapogushiwa.

Dk. Mhede ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 25 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya wamiliki wa viwanda wa mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na FCC kwa lengo la kukuza uelewa kuhusu udhibiti wa bidhaa bandia.

Dk. Mhede amesema wafanyabiasha wana jukumu la kufuatilia bidhaa zao sokoni na kutoa taarifa kwa tume hiyo pale wanapobaini uwapo wa bidhaa bandia zinzazofanana na bidhaa zao halisi.

“Tumieni fursa ya uwapo wa Tume ya Ushindani ili kuhakikisha kuwa ‘brands” (nembo za biashara) zenu zinalindwa. Nitoe wito kwa wamiliki wa viwanda na wawekezaji nchini kusajili alama za bidhaa zao ili bidhaa hizo ziweze kulindwa ziwapo sokoni” amesema Dk. Mhede.

Amesema Wizara itaendelea kuijengea uwezo tume hiyo ili wawekezaji wazidi kuwa na imani kuwa bidhaa zao zitalindwa na kuwa na uhakika kuwa bidhaa zao zitakuwa endelevu.

Amesema licha ya tume hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali imefanikiwa kupamba na changamoto hizo ikiwamo ongezeko kubwa la watu wanaojihusisha na biashara ya bidhaa bandia na kuahidi kuwa wizara itaendelea kuijengea uwezo ili wawekezaji wawe na imani kuwa bidhaa zao zitalindwa na zitakuwa endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles