23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

“Wamiliki wa vibanda kwenye masoko Simiyu ni Viongozi”-Takukuru

Na Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu imesema kuwa vibanda vingi kwenye masoko ya Halmashauri za Wilaya ya Maswa, Meatu na Bariadi vinamilikiwa na viongozi.

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu Aron Missanga akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya shughuli zinazotekelezwa na taasisi hiyo.

Aidha, taasisi hiyo imesema kuwa baadhi ya viongozi wanamiliki vibanda zaidi ya kimoja kwenye masoko hayo na kuvitumia kwa kujinufaisha wenyewe tofauti na malengo ya Serikali ya kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wale wa kati.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo kwa miezi mitatu kwa waandishi wa habari Machi 3, 2023 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa, Aron Missanga, amesema kuwa uchunguzi walioufanya umebaini kuwa viongozi hao walitumia madaraka yao vibaya kwa kuhodhi vibanda hivyo.

“Tulichobaini ni kuwa baadhi ya viongozi ndiyo wamiliki wa vibanda hivyo, tena wanamiliki vibanda viwili hadi vitatu, kisha wanawapangisha wafanyabishara kwa bei kubwa, na wanalipa kiasi kidogo kwenye halmashauri huku wakichukua kiasi kikubwa kwa wafanyabishara.

“Lengo la serikali kujenga masoko haya ni kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wao wapate sehemu za kufanyabiashara wajipatie kipato kwa gharama nafuu, lakini hilo haliko hivyo kwenye masoko yetu, vibanda vingi vimehodhiwa na viongozi,” amesema Missanga.

Amesema katika uchunguzi wa mfumo wa upangishaji wa masoko hayo, baada ya kubaini jambo hilo waliwaita wamiliki wa soko ambao ni halmashauri kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Amesema baada ya kuwaita wamiliki, walikaa kikao na kufanya mazungumzo kisha kuweka maazimio, ambayo ameeleza Halmashauri wametakiwa kwenda kuyafanyia kazi kadri walivyokubaliana.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo imesema kuwa ndani ya pindi hicho jumla ya kesi 8 ambazo ilizifikisha mahakamani na kutolewa uhamuzi, kati ya hizo 7 takukuru ilishinda huku ikishindwa kesi moja.

Taasisi hiyo imesema kuwa hatua hiyo ni mafanikio makubwa ambayo imepata, kutokana na umahili na ubora wa waendesha mashtaka waliopo kwenye taasisi hiyo lakini pia kufanyika uchunguzi ulio bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles