24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki wa mabasi waivimbia Sumatra

Na Asifiwe George, Dar es Salaam
WAMILIKI wa mabasi yaendayo mikoani wameitunishia msuli Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na kusema hawatashusha nauli kutokana na bei ya mafuta kuzidi kupanda.
Pia wamesema kama Sumatra hawatatoa majibu mapema, kuanzia Aprili 29 mwaka huu hawatokata tiketi kwa wasafiri wa mikoani badala yake wataitisha mgomo ambao utadumu kwa siku saba.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa) Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Enea Mrutu alisema Sumatra ilikurupuka kushusha nauli bila kufanya mchanganuo wa kina.
Pia wamiliki hao waliafikiana kuwa yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara kabla hawajapata mwafaka kutoka Sumatra watamchukulia hatua za kisheria.
Mrutu aliitaka Serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani kama ilivyokuwa awali kwa sababu bei ya mafuta imerudi juu baada ya kushushwa kwa kisingizio cha bei ya mafuta kushuka.
Pia wamiliki hao walizungumzia kukithiri kwa ajali za barabarani tangu Januari mwaka huu ambapo walijadili na kuafikiana kwamba kuanzia Mei Mosi mwaka huu watatumia mfumo uliopendekezwa na Serikali wa kuwapo kwa vituo maalumu vya kubadilishia madereva kwenye mabasi ya masafa marefu kwa muda wa miezi mitatu kwa majaribio.
Vituo hivyo vitakuwa Singida kwa mabasi ya Dar es Salaam kwenda Mwanza, Bukoba, Kahama na Kituo cha Morogoro kwa mabasi yanayokwenda mikoa ya nyanda za juu kusini.
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na mapendekezo ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, kuwa uchovu kwa madereva ndio chanzo kikuu cha ajali, hivyo kuhimiza uwapo wa madereva wawili wanaopokezana kwenye kituo kilichoteuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles