24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wami/Ruvu watakiwa kasi ya usimamizi wa raslimali maji

Na Ashura Kazinja, Morogoro

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi((CCM) Taifa, Daniel Chongolo ameiagiza Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu kuongeza kasi katika usimamizi wa rasilimali za maji kwa kupanda miti katika maeneo ambayo yameshaanza kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Chongolo ameyasema hayo Februari 6, 2023 mjini Morogoro baada ya kuzindua vitalu vya miche ya miti ya aina zaidi ya 10 vilivyoandaliwa na Bonde la maji Wami Ruvu, na maeneo yote ya pembezoni mwa mito ndani ya bonde hilo.

Amesema kupanda miti pembezoni mwa vyanzo vya maji kutasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo na kufanya mto kutokuwa hatarishi kwa wakazi wa mita 1,000 kutoka kilipo chanzo cha maji.

Aidha, amewataka bonde la Wami/Ruvu kutoa elimu kwa jamii inayoishi hadi mita 1,000 toka kilipo chanzo cha maji ili kujenga tabia ya kupanda miti itakayozuia mmomonyoko wa udongo na hivyo kujikuta wakiishi mahali salama.

Hata hivyo, alilipongeza Wami/Ruvu kwa kuandaa shamba la vitalu vya miche ya miti ya kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji ambapo aliwashauri kuwa na miti mingi zaidi ili watu binafsi na taasisi waweze kuipata na kupanda katika maeneo yao.

Hivyo, aliutaka uongozi wa bonde la maji Wami Ruvu kusimamia uundwaji vikundi vya watunzaji mazingira ili kuendeleza shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.

“Uharibifu wa mazingira ni mkubwa sana kwa sasa, na unasababisha kuwa na vipindi vya maji mengi kwa muda mfupi tu, na upungufu wa maji na ongezeko la wastani kwa muda mchache,” amesema Chongolo.

Awali Mkurugenzi wa Bonde la maji Wami Ruvu, Elibariki Mmasi alisema Bonde Wami/Ruvu linaendelea kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti pembezoni mwa mito huku likijiandaa kutangaza mto Ruvu kuwa eneo oevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles