31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wambura afikishwa mahakamani, asomewa mashtaka 17, yamo ya utakatishaji fedha

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Michael Wambura, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 17, yakiwamo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha zaidi ya Sh milioni 100.

Wambura amesomewa mashtaka hay oleo Jumatatu Februari 11 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina na Wakili wa Serikali, George Barasa.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo katika ofisi za TFF, kati ya Julai mwaka 2004 na mwaka 2015.

Barasa amedai Julai 7, mwaka 2004, Wambura alighushi barua akaiwasilisha TFF akijifanya barua hiyo imeandikwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jek System Limited ikidai malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000  zilizokopwa na TFF pamoja na riba.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka ya kughushi na mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka TFF akijifanya ni malipo ya mkopo na riba.

Wambura anadaiwa alijipatia fedha hizo kwa nyakati tofauti na anashtakiwa kwa mashtaka mawili ya kutakatisha fedha ambapo, kati ya Agosti 15 na Oktoba 24 alitakatisha Sh 25,050,000 na 75,945,024 huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles