Wambach akiri kutumia madawa kwenye soka

0
664

Abby WambachNEW YORK, MAREKANI

MCHEZAJI wa soka wa zamani wa timu ya Taifa ya wanawake ya Marekani, Abby Wambach, amekiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine pamoja na uvutaji wa bangi kwa ajili ya kusisimua misuli.

Wambach aliwahi kuwa mshindi wa kombe la dunia la wanawake na michuano ya Olimpiki mara mbili, alikamatwa siku ya Jumamosi kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Mchezaji huyu wa zamani alifikishwa Mahakamani siku ya Jumanne wiki hii katika Mahakama ya Multnomah County Circuit.

Katika nyaraka za mahakama hiyo, zimeandikwa kuwa alianza kutumika bangi akiwa na umri wa miaka 24 na matumizi yake ya mwisho ilikuwa saa 25 zilizopita kabla ya kukamatwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

“Kuna wakati ukifika mtu unatakiwa kuwa mkweli, nataka kila mmoja aamini ambacho ninakisema juu ya maisha yangu.

“Nilikuwa natumia madawa aina ya cocaine wakati nacheza soka kabla ya kustaafu, lakini hadi sasa natumia bangi, nimeamua kuyaweka wazi haya baada ya kukamatwa,” alisema mchezaji huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here